logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize avunja kimya kuhusu madai ya kurudiana na Kajala

“Kuanzia leo sitaki jina wala sura yangu iwekwe mahali fulani na msichana mrembo ambaye unadhani naweza kuwa naye," alisema.

image
na SAMUEL MAINAjournalist

Dakia-udaku28 October 2024 - 11:27

Muhtasari


  • Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alisema kuwa hajafurahishwa na kuhusishwa na wanawake wengine baada ya kuachana na mpenzi wake Poshy Queen hivi majuzi.
  • Staa huyo wa bongo fleva alibainisha kuwa sasa anachukua muda wake kabla ya kuchukua hatua ya kuingia kwenye uhusiano mwingine.

Staa wa Bongo, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize kwa mara ya kwanza amezungumzia taarifa ambazo zimekuwa zikivuma kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake Frida Kajala Masanja.

Akizungumza kwenye kipindi cha moja kwa moja kwenye mtandao wa Instagram, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alisema kuwa hajafurahishwa na kuhusishwa na wanawake wengine baada ya kuachana na mpenzi wake Poshy Queen hivi majuzi.

Mwimbaji huyo alibainisha kuwa wale wanaomhusisha na wanawake mbalimbali wanamfanya aonekane kama zuzu.

"Sipendi kabisa hali ambayo ninyi nyote mmekuwa mkinifanya nionekane kama zuzu. Nimeona kwenye mitandao ya kijamii, blogu na TV zikisema blablabla sijui Harmonize ataenda kwa fulani atarudi kwa fulani. Sijui itakuwa hivi na hivi,” Harmonize alisema.

Aliongeza, “Sikiliza, ninashukuru nyinyi watu kuzungumza kunihusu, sichukii hilo. Ninachukia tu ukweli kwamba nyinyi mnanifanya nionekane kama zuzu ambaye anaweza tu kuamka asubuhi moja na kuhama kutoka uhusiano mmoja hadi mwingine.”

Staa huyo wa bongo fleva alibainisha kuwa sasa anachukua muda wake kabla ya kuchukua hatua ya kuingia kwenye uhusiano mwingine.

Aliendelea kutuma onyo kali kwa watu dhidi ya kumhusisha na wanawake wengine yeyote.

“Kuanzia leo sitaki jina wala sura yangu iwekwe mahali fulani na msichana mrembo ambaye unadhani naweza kuwa naye.

Uhusiano ni maisha, ambaye unapaswa kuwa naye huamuliwa na maisha. Ninachukua muda wangu tu kuona ninapokosea na wapi ninaenda sawa. Nahitaji kujifunza zaidi,” alisema.

Hisia za Harmonize zinakuja baada ya siku kadhaa za mwimbaji huyo wa bongo fleva kudaiwa kupanga kurudiana na muigizaji Kajala Masanja.

Kumekuwa na madai kuwa bosi huyo wa Konde Music Worldwide kote umeendelea baada ya kuachana na sosholaiti Poshy Queen wiki kadhaa zilizopita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved