Wapenzi mashuhuri Peter Mwangi almaarufu Miracle Baby na Carol Katrue wamethibitisha kuwa hawako pamoja tena baada ya kuchumbiana kwa miaka kadhaa.
Wawili hao walithibitisha kuachana kwao siku ya Ijumaa jioni wakati wakiwafahamisha mashabiki wao kwamba sasa kila mmoja anafanya kazi kivyake.
Katika taarifa yake, Carol Katrue alitangaza kuwa sasa yuko single na hafanyi kazi na mtu yeyote.
“Niko single!! Kwa bookings nidm mimi tafadhalisifanyi kazi na mtu yeyote au chini ya mtu yeyote,” Katrue aliandika kwenye Instagram.
Kwa upande wake, Miracle Baby aliweka wazi kuwa hayuko tena na mama wa mtoto wake mmoja na alitaka mtu yeyote anayemtafuta awasiliane naye moja kwa moja.
“Kwa yeyote aliyekuwa akinipigia simu kwa ajili ya show za Carol Katrue, hatupo pamoja tena!! asante,” Miracle Baby alisema.
Haya yanajiri miezi michache tu baada ya wanandoa hao kupitia wakati mgumu wakati Miracle Baby alipokuwa akipambana na ugonjwa mbaya ambao ulimfanya kufanyiwa upasuaji mara kadhaa. Carol alisimama waziwazi na msanii Mugithi na gengetone alipokuwa mgonjwa.
Mnamo Machi mwaka huu, Carol Katrue alifichua kiasi alichokuwa akitumia kila siku kumtibu baba ya mwanawe.
Katika mahojiano, alieleza kuhusu sharti ambalo mumewe Miracle Baby alikuwa nalo, akisema kwamba alikuwa akiwapigia simu Jaguar na KRG The Don mara kwa mara ili wamsapoti kwa kutuma pesa ili aone kimbele matibabu ya mumewe.
“Nilikua nashinda nkisumbua Jaguar namuitiosha doh hadi sa nane za usiku juu ikianza kuleak inaleta shinda, a kina KRG wote nimeshinda nikiwasumbua.
Ndio Jaguar akaenda kuongea na rais akatusaidia na pesa yenye alileta na ametusaidia... kwa siku ilikuwa Sh30, 000,” Carol Katrue alisema.
Wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa miaka kadhaa sasa na wana mtoto mmoja pamoja. Miracle Baby hata hivyo ana watoto wengine wanne na wanawake tofauti.