Aliyekuwa msanii katika kundi la Sauti Sol Bien, amemtania msanii mwenzake Khaligraph Jones kuwa mlinzi wake katika video ambao Jones maarufu kama OG alichapisha kwenye mtandao wake wa Instagram.
Mnamo Jumatano, OG alichapisha video ambapo wawili hao walikuwa wanatembea katika nyumba moja ambapo Bien alifungua mlango kisha OG akamfuata nyuma. Kwenye video hiyo, OG amevalia kabuti kubwa jeusi pamoja na viatu vya rangi sawia vinavyovaliwa sana na walinzi wa watu mashuhuri.
Mseto wa maoni kutoka kwa wafuasi ulifurika kwenye chapisho hilo, jumbe nyingi zikiwa za utani kwa OG.
Bien kwa upande wake alimtania OG kwa kumtaja kuwa mlinzi wake.
“Once a bouncer always a bouncer. Usalama leo ulikuwa imara.” Alisema Bien.
Aidha mbali na maoni ya Bien, wafuasi wengine waliandika maoni yao ya kutania msanii huyo wa Rap nchini.
“Utashangaa hiyo sehemu ya kuegesha magari iko jikoni kwa OG.” Alisema mtumizi mmoja wa instagram huku OG akimjibu kwa emoji za kucheka.
Hata hivyo, Khaligraph Jones alitishia kuondoa video hiyo mtandaoni baada ya mtumiaji mmoja wa Instagram kutoa maoni yake akiuliza ikiwa Bien alikuwa na mlinzi wake kwenye video hiyo.
“Huyu
ni Bien na mlinzi wake ama?” Aliuliza ianomistah
Jones
alimjibu kwa kusema atafuta video hiyo kutoka. “wacheni madharau bana, lakini pia
me nimeona inakaa hivo, nitafuta video hii.” Alisema Khaligraph Jones.