Mwakilishi wa wananchi wa eneo bunge la Mumias Mashariki Peter Salasya amekiri kuwa katika maisha yake pesa ni kama maua.
Mbunge huyo ambaye anahudumu katika bunge la kitaifa kwa mara kwanza amesema kuwa kuandaa mashindano ya kabumbu chini ya jina lake ni rahisi huku akiomba Mungu amsaidie kufanikisha shughuli hiyo.
Imekuwa ni ada kwa wanasiasa nchini Kenya kuandaa mashindano haswa ya kabumbu katika maeneo wanayotoka kama njia ya kuwahamasisha vijana ambao ni wanafunzi kutojihusisha katika maswala ya utovu wa nidhamu wakati shule zimefungwa. Vile vile, wanasiasa hutumia fursa hiyo kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wapiga kura.
Aidha kwa upande wa mbunge Peter Salasya, amekiri kuwa ili kuandaa mashindano yenye mafanikio, sio mchezo huku akiomba Mwenyeji Mungu kumsaidia katika kukamilisha shindano ambalo ameandaa katika enbeo bunge lake.
Hata hivyo mbunge huyo amesema kuwa bajeti ya kufanikisha shughuli hiyo ni ghali mno japokuwa ameamini kuwa Mungu atamsaidia akisema kuwa kwake pesa ni maua.
“Kuwa na mashindano yenye mafanikio sio kitu cha utani, Mungu naomba unisaidie. Bajeti iko juu lakini Mungu ni nani. Atafanikisha vizuri kwangu pesa ni maua.” Aliandika Salasya kwenye ukurasa wake wa IG.
Mashindano ya PK Salasya classic cup yalianza rasmi Jumapili Disemba mosi na yanatarajiwa kukamilika Januari mosi kwa fainali.
Mbunge Salasya aliwasili katika eneo bunge lake kuzindua
rasmi mashindano hayo kupitia Kisumu alikoshuka kwa ndege kutoka Nairobi.