Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nadia Mukami amefichua kwamba ikiwa hangelikuwa kwenye mahusiano na msanii mwenzake Arrow Bwoy, angalikuwa kwenye mahusiano na Stevo Simple Boy ambaye pia ni msanii wa muziki.
Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha burudani cha mtandaoni nchini Kenya, msanii huyo wa kibao cha Roho Mbaya, amesema kwamba Stevo Simple Boy ana uwezo wa kumpiga ‘kompe’ Arrow Bwoy ambaye ni mumewe.
“Mimi napenda Stevo sana, Arrow Bwoy hangekuwa Stevo angepata chance. Stevo anaweza kupiga ‘kompe’. Alisema Nadia Mukami.
Nadia alisema kwamba Stevo anaweza na huwa anamchekesha sana.
Kwa upande wa Arrow Bwoy aliyekuwa pamoja na mkewe kwenye mahojiano hayo, alitania kwamba Stevo anaweza kumtafuta ili wafanye maongezi kuhusu Nadia akisema kwamba katika dunia ya sasa inawezekana.
“Tuko modern World kuja tuongee. Kuja tukuwe wawili” Alisema Arrow Bwoy.
Hata hivyo, wana ndoa hao ambao wamejaliwa mtoto mmoja,
wamemtia moyo msani Stevo Simple Boy kwa mistari yake na misemo ambayo huwa
anatoa. Arrow Bwoy alisema kwamba Stevo huwa anawajenga sana huku akimtaka atoe
nyingine.
“Stevo anatujenga, bro endelea hivo hivo. Toa
ingine.”
Alisema Arrow Bwoy.