Sosholaiti maarufu kutoka Uganda Zari Hassan amesherehekea kumaliza mwaka wa 2024 pamoja na mume wake Shakib Cham Lutaaya.
Katika chapisho la Alhamisi jioni, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 44 hata hivyo alikiri kwamba ndoa yao imekumbwa na changamoto nyingi mwaka jana.
Zari alidokeza kwamba waligombana sana, wakanyamaziana kimya, na kuachana mara kadhaa kadri mwaka ulivyosonga.
"Kumaliza mwaka na wewe baada ya talaka milioni 1 kwa wiki, kukunjiana uso mara 7 kwa siku na mapigano 3 ya kimya kwa mwezi," Zari alisema.
Aliendelea kusisitiza upendo wake usio na mwisho kwa kijana huyo wa miaka 33.
‘Nakupenda milele kuenda,” aliongeza.
Mama huyo wa watoto watano aliambatanisha taarifa yake na picha yake na Shakib ndani ya bwawa la kuogelea.
Mwezi Agosti mwaka jana, Zari alizamia kwenye mitandao ya kijamii kumzomea mumewe Shakib na kutishia kumuacha. Hii ilikuwa baada ya Shakib kuonyesha kutilia shaka uhusiano wa Diamond na mkewe.
Katika kipindi cha moja kwa moja kwenye mtandao wa kijamii, mama huyo wa watoto watano alifichua kuwa mumewe hana uhakika kuhusu ndoa yao na amekuwa akihoji uhusiano kati yake na mzazi mwenzake, Diamond Platnumz.
Zari alisema alilazimika kufanya kipindi cha moja kwa moja ili kueleza wazi kuwa yeye na Diamond hawako kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi, ili tu kumhakikishia mumewe kuhusu auaminifu wake katika ndoa yao
“Ngoja niwaambie kitu, Nikitaka kumrudia Diamond naweza kurudi. Ikiwa Diamond anataka kunirudia, anaweza kurudi. Lakini sisi tumemalizana. Sisi tumemalizana kabisa. Simtaki, hanitaki,” Zari alisema Jumapili usiku.
Sosholaiti huyo aliweka wazi kuwa ana mume na mzazi mwenzake pia ana mpenzi.
“Mume wangu hajiamini sana, na hilo linaleta matatizo mengi. Lazima niwe hapa kuelezea. Kweli? Boss lady mzima, inabidi nifanye kipindi chote cha moja kwa moja, ili tu kuthibitisha uhakika kwa mume wangu. Kipindi hiki ni kuthibitisha kitu kwa mume wangu,” aliongeza.
Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 43 alibainisha kuwa ana sifa zote nzuri na anaweza kuwa na mtu yeyote ambaye anataka kuwa naye.
"Lakini nilimchagua mume wangu, na sijali jinsi nyinyi mnamwona. Ooh, amefilisika, hafai vya kutosha, sijali. Nilimchagua. Nilichagua kuwa naye kama mume wangu, kisha ananiweka katika hili!!,” alisema.
Zari alidokeza kuwa mumewe hana budi kuacha kutokuwa na uhakika kuhusu ndoa yao ikiwa anataka iendelee vyema.