Mwanamziki kutokea
Tanzania Harmonize ametoa onyo la hatari kwa wale wanamdhalilisha mchumba wake
mpya Abby Chams..
Alisema kuwa anampenda sana mwanamke wake na mtu
yeyote hafai kumzungumzia visivyo.
“Niko
kiukweli kabisa kuhusu hili, sitaki kusikia chochote kuhusu mchumba wangu. Wanablogu na wanahabari msitaje mchumba wangu kwa mambo mabaya yasiyo na heshima,
hilo linaniumiza sana, linapofika masikioni
mwangu. Alisema mwana mziki huyo aliyeimba kibao kinachotrend kwa sasa. “
MATATIZO”
Abby Chams
ambaye jina lake halisi Abigail Chamungwana pia ni mwanamziki ambaye amefanya collabo
na wasani wakubwa tokea Tanzania akiwemo Ali Kiba na boyfriend wake wa sasa
Harmonize.
Wawili hao
walianza mahusiano yao muda mchache baada ya harmomize kumuhusisha katika wimbo
wake wa “ Closer”, mwaka jana 2024.
Hao wanamziki
walianza mahusino yao rasmi baada ya Harmonize kutangaza hadharani kuachana na
mchumba wake wa zamani Poshy Queen Oktoba mwaka jana. Hata hivyo mwanamziki
huyo amedinda kuzungumzia kuhusu swala lililomfanya yeye kutengana na mchumba
wake huyo wa zamani. Wawili hao walitengana baada ya kuwa kwa mahusiano kwa
miaka miwili.
“Niko macho
naona kila kitu ambacho kinazungumziwa katika mahusiano yangu mapya. Niaminini sijafurahia.
Siwezificha kile ambacho nimekiweka hadharani. Kimya changu ni kwa sababu
sitaki watu wazungumze mambo tofauti. Heshima yang kwa famila yao ni kubwa sana
na hatujafaulu kuwa pamoja milele. Tunafaa kuelewa kwamba kila kitu hupangwa na
mwenyezi Mungu,” Harmonize alielezea hili kuhusu mapenzi yake ya zamani.
Kwa sasa Star
huyo wa bongo Tanzania amemteuwa mpenzi wake huyo wa zamani Poshy Queen kama
afisa mtendaji [ CEO] wa kampuni yake ya kamari [betting company] inayojulikana
kama Bukua Milioni.