KISA cha kushangaza kilishuhudiwa katika mahakama moja nchini Nigeria baada na mwanamke mmoja kupandishwa kizimbani kwa shtaka la ulaghai na utapeli.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Naija PR nchini humo, mwanamke huyo alikamatwa kwa kudanganya kuhusu hali yake ya kimapenzi.
Mwanamke huyo, ambaye ameolewa anasemekana kudanganya mwanamume mwingine kwamba yeye hana mume na kuchukua pesa zake lakini akakataa kuolewa naye.
Inaarifiwa kwamba mwanamke huyo alikusanya jumla ya Naira 607,500 (Ksh52,300) kutoka kwa mwanamume huyo wa pili kwa njia ya ulaghai baada ya kumwambia kwamba yeye hakuwa na mume.
Jamaa baada ya kutumia pesa zake kwa mwanamke huyo aliyemwambia yuko single, ulifika wakati akamuomba waoane lakini mwanamke huyo aliibuka na visingizio maradufu.
Jamaa huyo alichoka na visingizio vyake na akazama kufanya uchunguzi kubaini ni kwa nini ‘mchumba’ wake hakuwa anataka kuolewa naye.
Kwa mshangao wake, aligundua kwamba mwanamke huyo alikuwa mke wa mtu na ndio sababu hakuwa anataka kuolewa na huyo jamaa wa pili licha ya kuchukua pesa zake na kumdanganya kwamba hana mume wala mpenzi.
Chapisho hilo lilivutia maoni mseto kwenye mitandao wa X lilikochapishwa.
“Polisi wamemfikisha mahakamani mwanamke wa mtu kwa kukataa kuolewa na mwanaume mwingine baada ya kudai kuwa hajaolewa na kumlaghai N607, 500 kutoka kwake,” sasisho hilo lilisoma.
Haya hapa ni baadhi ya maoni ya kushangaza;
@Bartezz10: “Kwa hivyo sasa anapaswa kuolewa naye kwa nguvu au nini kitatokea kwake?”
@anasuachara: “Hataki kutenda kosa la Bigamy. Ndio maana alikataa kuolewa na mwanaume huyo kwa vile tayari alikuwa ameolewa.”
@OgechukwuIgboa2: “Chia, jinsia hiyo eeh. Gereza moja kwa moja au ulipe pesa na faini.”
@uzoma_okey29800: “Vitendo vya Ulaghai Vinakuja Kwa Mifumo Tofauti Siku Hizi! Na Swali Bado Limebaki Je Tumefikaje Hapa??”
@Gossipfxboi: “Wanaume Wanashinda Kesi za Mahusiano Siku hizi Je, ni Athari ya rais Siku hizi?