
MABINTI 3 wanashikiliwa na polisi baada ya kudaiwa kumteketeza moto hadi kufa nyanya wao mwenye umri wa miaka 96 wakimtuhumu kuwa sababu ya wao kutoolewa na wanaume matajiri.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mkoa wa Mashariki nchini Zambia,
mabinti hao 3 walichoma bibi yao wakimtuhumu kwa kuwaroga ili waangukie katika
ndoa za wanaume fukara.
Tukio hilo lilitokea Jumatatu katika Kijiji cha Malama kati
ya saa saa tatu na saa tano usiku.
Miongoni mwa washukiwa hao watatu, mmoja ni msichana mkubwa
mwenye umri wa miaka 29 huku wenzake wawili wakiwa ni matineja wa miaka 18 na
19 mtawalia – wote wajukuu wa bibi huyo ambaye sasa ni marehemu.
Watatu hao walitekeleza tukio hilo kwa pamoja wakimchoma hadi
kufa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 96 kwa mapazia kwa kutumia nyasi
walizokusanya kutoka kwa jiko lililoezekwa kwa nyasi ambalo liko umbali wa mita
saba kutoka eneo la uhalifu, chombo kimoja cha habari kilieleza.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Ofisa Mnadhimu wa
Polisi Mkoa wa Mashariki, Robertson Mweemba aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Tamara
Mazyopa 29, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 18 na Beatrice Nyoni mwenye umri
wa miaka 19 wote wa kijiji cha Chipeni.
Bw. Mweemba alisema uchunguzi ulibaini kuwa mauaji hayo
yalianzishwa na Tamara Mazyopa, ambaye ni mjukuu mkubwa.
Baada ya kumchoma moto marehemu katika nyumba yake yenye
vyumba vitatu, watatu hao walifunga mlango ili asipate nafasi ya kuishi.
Kamanda wa Polisi alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ukisubiri kufanyiwa uchunguzi
huku watatu hao wakisota kwenye seli wakisubiria kufunguliwa mashtaka ya
mauaji.