Kajala akizungumza na mwanahabari Mwijaku ameelezea kwamba kuvunjika kwa mahusiano hayo kumemfanya kuamini kwamba uchawi upo.
Mwijaku aliweka wazi haya wakati wa kipindi chake kupitia redioni baada ya kukutana na mwigizaji Kajala huku muigizaji huyo akionekana kuchanganyikiwa na maamuzi ya maisha yake.
"Bwana jana nilipata bahati ya kuongea na Kajala. Kitu ambacho Kajala mpaka sasa hivi hakielewi, anasema haelewi kitu gani kilifanya aachane na Harmonize. Kajala kitu ambacho amesema mpaka leo, anasema uchawi upo. Sielewi kitu gani kilinifanya niachane na Harmonize," Mwijakuu alinikuu maneno ya kajala.
Mwigizaji Kajala pia aliweka wazi kwamba hawakuwahi kukosana kabla ya siku hiyo ya kuwaachana. Amesisitiza kwamba waliachana pasiposababu, kwani hakuna aliyewahi kumufumania mwingine.
Kajala aleleza kwamba kuilikuwepo na kudekadeka kidogo tu na akatania kwamba anaondoka na hivyo ndivyo vitu vilibadilika na kuwa halisi.
"Niamka nikasema kwamba nachukua vitu vyangu naenda naye akaniambia niende. Hakukuwa na ugomvi baina yangu na yeye," alisema.
"Mimi sielewi kilichotokea kabisa labda umuulize rafiki yako, hajanifumania, sijamfumania, yaani kuna pepo iliinghia asubuhi tu mara moja ondoka ukachukue vitu zako na hivyo ndivyo kukawa, ikaisha hapo mpaka leo. Kajala alimwelezea Mwijaku.
Kajala amefichua kujutia kuvunjika kwa mahusiano hayo ila yalishamwondokea. " Ndani ya nafsi yake anakwambia kabisa kamwe hawezi kuyasahau maisha yale. Siwesi kudanganya kusema eti huyu nimemsahau, ana mema yake mazuri," alieleza.
Kajala hata hivyo amesema kwamba hana imani iwapo anaweza kurudi katika mahusiano hayo na kueleza kwamba kwa sasa hajui moyo wake kiukweli unataka nini.
Kajala na Harmoniza walikuwa kwenye mahusia kwa muda angalau miezi mitatu.