
MWANAMKE mmoja mwenye umri wa miaka 37 aliishangaza mahakama ya kusuluhisha migogoro ya ndoa baada ya kuwasilisha ombi la talaka kutoka kwa mumewe akidai anampelekea moto mkali.
Kwa mujibu wa Vanguard, mwanamke huyo kutoka jimbo la Kaduna
nchini Nigeria alielezea mahakama kwamba amechoka na ndoa yake kwa sababu
mumewe anafanya mapenzi naye kila siku usiku kucha bila kuchoka na hampi muda
wa kupumzika.
Alisema kwamba amejaribu kuvumilia lakini ameona ni kama
anaumia kwani amefika mwisho na katu hawezi kustahimili kiu cha mapenzi cha
mumewe.
Katika ombi lake, Bi Linda, pia alimshutumu mumewe kwa
kumpiga kila alipokataa matamanio yake ya kufanya mapenzi, jambo ambalo
limemfanya kuona ndoa ya miaka 6 kuwa chungu.
Aliambia mahakama kuwa havutiwi tena na ndoa hiyo kwani
hawezi tena kustahimili hitaji la kupita kiasi la mumewe.
"Ninaiomba mahakama kuvunja ndoa hii kwa sababu siwezi kustahimili
hamu yake ya kujamiiana kupita kiasi. Anapenda mapenzi kupita kiasi, na siwezi
kuvumilia.”
"Mara nyingi alikuwa akifanya mapenzi na mimi kuanzia usiku wa
manane hadi alfajiri, hata nikilia haachi.”
"Imepita miezi mitatu tangu nihame nyumbani kwake, ndugu zake
wamekuwa wakinisihi nirudi kwake, lakini hawajui ninachokabiliana nacho,"
alisema.
Alisema zaidi kwamba mume wake hajidhibiti wakati wowote
anapohitaji mapenzi, na kwamba wakati wowote alipokataa matamanio yake ya
kufanya mapenzi, alikuwa akimpiga, hata mbele ya watoto wao wawili.
Stephen, Mumewe katika majibu yake, aliiambia mahakama kuwa
anampenda mkewe na bado anamhitaji.
Stephen alisema amekuwa akimsihi mke wake asitake talaka,
kwani sasa yuko tayari kudhibiti hamu yake ya kujamiiana.
"Niliwapeleka wajomba na marafiki nyumbani kwa wazazi wake ili
kumsihi. Lakini alikataa kutusikiliza badala yake alituacha,"
Stephen alisema.
Aidha aliiomba mahakama kumpa muda wa kurekebisha mambo na
kurudiana na mkewe.
Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 6 kwa ajili ya kupata
mrejesho na matokeo ya maridhiano hayo huku akiwashauri kudumisha amani.
Ni kesi ambayo imevutia usikivu wa wengi haswa mitandaoni,
baadhi wakidai kwamba hamu ya mapenzi ya mume huyo ni ndoto na tamanio la
wanawake wengi huku wengine wakidai kwamba huenda alikuwa anatumia dawa za
ziada za kuongeza nguvu na hamu yake.