Kumzalia Diamond? Zuchu azungumzia uwezekano wa kupata mimba mwaka huu

Mahusiano ya msanii huyo wa WCB yamesalia kitendawili baada ya kudaiwa wameachana na Diamond.

Muhtasari

•Zuchu ambaye alionekana waziwazi kutopenda kabisa utabiri aliopewa alisema, "Hell naaaaaw to noo!"

•Zuchu alisema kusalitiwa kimapenzi si hoja bali hoja ni  mpenziwe kumletea mwanamke mwingine katika nyumba yake.

Zuchu na bosi wake Diamond
Image: HISANI

Malkia wa Bongo Zuhura Othman Kopa almaarufu Zuchu amefutilia mbali uwezekano wa kupata ujauzito mwaka huu wa 2023.

Hivi majuzi, msanii huyo wa WCB alishiriki katika challenge ya Tiktok ambapo ilitabiriwa jinsi mwisho wa mwaka ungempata mtu.

Kwa mshangao wake Zuchu, mtabiri alionyesha kuwa ana uwezekano wa kuwa mjamzito ifikapo Desemba mwaka huu.

Zuchu ambaye alionekana waziwazi kutopenda kabisa utabiri aliopewa alisema, "Hell naaaaaw to noo!"

Kumaanisha: "Hapana kabisa!"

Haya yanajiri katika kipindi ambapo mahusiano ya binti huyo wa  gwiji wa taarab, Khadija Kopa yamebaki kuwa kitendawili.

Kwa muda mrefu, mtunzi huyo wa kibao  ‘Sukari’ alidaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na bosi wake Diamond Platnumz hadi mapema mwaka huu ambapo wawili hao walijitokeza kudai kwamba wameachana. 

Mwezi Februari, Diamond Platnumz aliweka wazi kwamba yeye na Zuchu sio wapenzi tena. Alibainisha kuwa yeye na malkia huyo wamebaki kuwa kaka na dada licha ya awali kuonyesha mahaba  makubwa kati yao.

"Kwa pamoja na Zuhura tunaomba tuwataarifu ya kwamba, kwa sasa sisi ni dada na kaka na si wapenzi kama ilivyokuwa ikidhaniwa ama wengine kujua.. Mnaruhusiwa wachumba na wake ama waume kama tutawaridhia," alisema.

Diamond aliongeza, "Lakini muwe na vibarua vinavyoeleweka  sio mje kutuchuna, maana atuhongi hovyo."

Mapema mwezi huu, Zuchu alionekana kujawa na ghadhabu baada ya Diamond kuonekana akimbusu kimahaba mwanamke mwingine katika sehemu ya pili ya filamu halisia ya Young, Famous na Africa.

Siku moja tu baada filamu  hiyo kupeperushwa kwenye Netflix, msanii huyo wa lebo ya WCB  alichapisha picha zake kadhaa kwenye Instagram. Pamoja na picha hizo, aliambatanisha video fupi ya mwanamuziki akiimba maneno ya matusi mazito mazito ambayo yalionekana kuelekezwa kwa Diamond.

Binamu yake Diamond, Romy Jons alichukua hatua ya kumuuliza binti huyo wa Khadija Kopa ikiwa tayari ameshaitazama.

"Umeangalia msimu mpya wa filamu ya Dai? " Romy Jons alimuuliza Zuchu.

Malkia huyo wa Bongofleva  aliyeonekana kukerwa na swali hilo alijibu, "Nimeangalia mwaya mwambie nimesema F++k you."

Baadaye hata hivyo, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 29 alidokeza kwamba hawezi kumuacha mpenziwe hata akimsaliti.

Zuchu lieleza kuwa kusalitiwa kimapenzi si hoja bali hoja ni  mpenziwe kumletea mwanamke mwingine katika nyumba yake.

Kucheat inategemea. Huwezi cheat mbele ya macho yangu nikakusamehe, hilo haliwezi tokea. Lakini ati umecheat zako huko makampepaka, nyumbani tukiwa wawili hehehe. Wewe utakaa huko na baby wako tutakutana nyumbani,” Zuchu alisikika akisema katika video iliyosambaa mitandaoni.