Mulamwah azungumzia wakati alipompiga Sonnie na mzee anayedai kuwa 'mubabaz' wake

Alidai kuwa vita ilianza baada ya mpenziwe Sonnie kumshtumu kwa kusambaratisha ndoa yake.

Muhtasari

•Mulamwah alisema aliwashambulia Sonnie na mwanamume mzee ambaye anadai kuwa mpenzi huyo wake wa zamani alikuwa amejitosa  kwenye mahusiano naye.

•Alikiri kuwa yeye na mzee anayedai kuwa mpenzi wa Sonnie walitoka katika hoteli  hiyo wakiwa na alama  za vita kila mmoja.

Carrol Sonnie na aliyekuwa mpenzi wake Mulamwah
Image: HISANI

Mchekeshaji David Oyando almaarufu Mulamwah amefunguka kuhusu wakati ambapo alihusika katika vita na mzazi mwenzake Carol Sonnie na mwanaume anayedai kuwa ni mpenzi wa muigizaji huyo.

Katika mahojiano na Presenter Ali, Mulamwah alisema aliwashambulia Sonnie na mwanamume huyo mzee 'mubabaz' katika mkahawa mmoja jijini Nairobi ambapo walikuwa wamekutana kwa ajili ya mazungumzo.

Alidai kuwa vita ilizuka baada ya mpenzi wa mzazi mwenzake kumshtumu kwa kusambaratisha ndoa yake.

"Nilikuwa nimekasirika. Alisema nimeingilia familia yake. Tulikuwa tunakunywa juisi hapo, jamaa akanilima na glasi, nikarudisha," alisimulia.

Alisema kuwa baada ya mwanaume huyo kumvamia alipandwa na mori na kusimama kisha vita kubwa ikazuka kati yao.

"Mimi sikutaka kujua kama huyo ni mubaba ama nini. Kalitamba vizuri. Ilikuwa vita nzuri ya dakika tatu, nne hivi," alisema Mulamwah. 

Mchekeshaji huyo alisema kuwa wenzao waliokuwa pale ndio waliotenganisha vita hiyo wakati ilipokuwa imechacha.

"Mimi kutenganishwa niliwekwa karibu na Sonnie. Nilikuwa nimekasirika sana,nilimsamba sana siwezi kataa. Nilimtandika vibaya kwa sababu kila mtu kwa hiyo nyumba alikuwa hapo kwa sababu yake," alisema.

Alikiri kuwa yeye na mzee anayedai kuwa mpenzi wa Sonnie walitoka katika hoteli  hiyo wakiwa na alama  za vita kila mmoja.

Hata hivyo alidai kuwa hayo yote yangeepukika ikiwa mpenzi huyo wake wa zamani angekuwa anasema ukweli.

"Mimi mpaka naanza kupigana na wazee mjini, kitu sijawahi kufanya maishani. Sijawahi kupigana na yeyote. Nilikuwa nimekasirika sana, hata nilikuwa naondoka hapo bila viatu kabla ya kuambiwa tuombe,"  alisema.

Alisema maombi yalifanyika kila mmoja akiwa amefungua macho kwani kulikuwa na hali ya taharuki katika kikao hicho.

Mapema mwezi jana Mulamwah alimshtumu mzazi mwenzake kwa kuchumbiana na mzee wa miaka 60 aliye kwenye ndoa nyingine tayari.

Alichapisha picha kadhaa za mpenzi huyo wake wa zamani na kutoa maelezo ya kuyapa nguvu madai yake.

"Mnakulana na wazee wa miaka 60 halafu mnakuja kuweka viwango kwenye mtandao na picha za kipuzi na mahojiano ya kupuzi,"

Baadae  alidai kuwa 'mubabaz' ambaye mzazi  huyo mwenzake alikuwa kwenye mahusaiano naye anatishia maisha yake.

Sonnie hata hivyo alijitokeza kupuuzilia mbali madai hayo na kueleza kuwa mwanaume ambaye mchekeshaji huyo alikuwa akizungumzia ni mhubiri wake.