logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Ujauzito ni rahisi kuliko baada ya kujifungua!' Nadia azungumzia masaibu ya baada ya kujifungua

Nadia amefichua kuwa miezi minne baada ya kujifungua mwanawe haijakuwa rahisi kwake.

image
na Radio Jambo

Makala25 July 2022 - 07:13

Muhtasari


•Nadia na mumewe Arrow Bwoy walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza pamoja mnamo Machi 24 mwaka huu.

•Kulingana na Nadia, kipindi cha ujauzito huwa rahisi kwa mwanamke kuliko kipindi cha baada ya kujifungua.

Malkia wa muziki nchini Kenya Nadia Mukami amefunguka kuhusu matatizo ya baada ya kujifungua.

Nadia na mumewe Arrow Bwoy walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza pamoja mnamo Machi 24 mwaka huu.

Mama huyo wa mtoto mmoja amefichua kuwa miezi minne baada ya kujifungua mwanawe haijakuwa rahisi kwake.

"Kipindi cha baada ya kujifungua sio mzaha! Sikuwahi kuelewa kabisa kuhusu kipindi cha baada ya kujifungua hadi nilipopata mtoto," Alisema kupitia Instastori zake.

Nadia  amebainisha kuwa kipindi cha baada ya kujifungua kwa kawaida huwachosha wanawake wengi.

Kulingana naye, kipindi cha ujauzito huwa rahisi kwa mwanamke kuliko kipindi cha baada ya kujifungua.

"Ujauzito ni rahisi! (Maoni yangu) nadhani ni rahisi ukilinganisha na kipindi kile baada ya kujifungua! Sheesh! Wanawake wana nguvu! Na sisi wanawake weusi/Waafrika haturuhusiwi kusema kipindi hiki kinachosha utaambiwa , leta mtoto ni/tulee kama amekushinda," Nadia alisema.

Msanii huyo mwenye kipaji kikubwa ametoa wito kwa watu kuwajulia hali kina mama wapya mara kwa mara.

Takriban miezi minne iliyopita, Nadia na Arrow Bwoy walimkaribisha  mtoto wao Haseeb Kai duniani.

"24.03.2022 tumepokea zawadi nzuri zaidi Haseeb Kai. Karibu kwenye ulimwengu wetu," Arrow Bwoy alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hapo awali wanandoa hao walikuwa wamepoteza ujauzito wa ambaye angekuwa mtoto wao wa kwanza.

Kupitia Youtube Channel yake, Nadia alifichua kwamba alipoteza ujauzito wake wa kwanza mnamo Aprili 12, 2021.

Alifichua kuwa alikumbwa na huzuni kubwa kutokana na tukio hilo la kutisha  hadi kulazimika kupata ushauri wa kisaikolojia.

"Ulikuwa wakati mgumu kuwahi pitia. Huo ndio wakati nilitamani singekuwa msanii. Hospitalini nilioshwa, nilipotoka bado nilikuwa na trauma. Nilipitia kiwewe hadi nikaenda kupata ushauri. Nilikuwa naenda kupata ushauri na watu hawakujua, huo ndio wakati nilikuwa natengeneza ofisi yangu. Nilishauriwa sana na ilisaidia sana," Nadia alisimulia.

Katika kipindi hicho, mama huyo wa mtoto mmoja alijaribu sana kuficha hisia zake na kujifanya kama kwamba yupo sawa.

Msanii huyo hata hivyo alibahatika kupata ujauzito mwingine takriban miezi miwili baada ya kupoteza ule wa kwanza


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved