Msijaribu! Najuta kufanya surgery - Munalove

Muhtasari

• Msanii kutoka Tanzania, Munalove amesema kwamba anajuta kufanya upasuaji ili kujiongezea baadhi ya sehemu za mwili wake.

• Munalove amewaonya mashabiki na watanzania wote kuepuka kutaka kubadilisha sehemu za miili yao akisema kwamba anapitia kipindi kigumu tangu afanyiwe upasuaji huo.

Munalove100
Munalove100
Image: Instagram KWA HISANI

Msanii kutoka Tanzania, Munalove amesema kwamba anajuta kufanya upasuaji ili kujiongezea baadhi ya sehemu za mwili wake.

Munalove amewaonya mashabiki na watanzania wote kuepuka kutaka kubadilisha sehemu za miili yao akisema kwamba anapitia kipindi kigumu tangu afanyiwe upasuaji huo.

Kupitia ujumbe aliochapisha katik ukurasa wake wa Instagram, Munalove ametoa ahadi kwa mashabiki wake kwamba karibuni atawaelezea aliyoyapitia tangu achukue hatua hiyo.

“Achananeni na surgery, msifanye ntakuja kuwaeleza vitu vingi ninavyopitia, nampenda sana Yesu,” aliandika Munalove.

Mwanadada huyo anaonekana kujutia kitendo hicho, jambo ambalo linaonekana kusambaratisha uhusiano wake na Mungu huku akitoa hakikisho kwamba amejirudi na sasa anampenda Yesu na kwamba atamtumikia daima.

Wasafi tv
Wasafi tv
Image: Instagram KWA HISANI

Munalove ambaye mwaka jana alifanya upasuaji wa dimples na mwili wake kiujumla anasemekana kupitia kipindi kigumu cha madhara yaliyotokana na upasuaji huo , jambo ambalo limempelekea kutoa ushauri kwa mashabiki wake kutojaribu kufuata mkondo huo.

Kwa sasa mashabiki wanasubiri kusikia kutoka kwake kuhusu kile alichokipitia baada yake kufanya upasuaji ili kubadilisha sehemu zake za mwili.