Mwimbaji mbilikimo kutoka Guinnea ni rasmi amedunda nje ya soko la kuchumbiana baada ya kuonekana kwenye video akipiga goti na kutoa ombi rasmi la ndoa kwa mpenzi wake wa muda mrefu kutoka Ivory Coast, mwanamitindo Eudoxie Yao.
Katika video hiyo ambayo Yao ameipakia katika ukurasa wake wa Instagram, Grand P anaonekana akimshikilia mkono kama vile anamvisha pete na kuenda chini kwa goti moja huku akitoa ombi lake la ndoa kwake katika lugha ya Kifaransa.
Eudoxie Yao amefurahia ombi hilo na kuonekana akimuinua na katika video hiyo amefuatisha na maneno kwamba ombi la ndoa kutoka kwa mpenzi wake wa zamani (Grand P) lilimfurahisha sana na kudokeza kwamba ana kazi ya kuifanya katika kuafikia maamuzi ambayo hatayajutia mbeleni. Na anaonekana kubaki kwenye njia panda kama bado anaweza kumuamini au la.
“Pendekezo la ndoa kutoka kwa mpenzi wangu wa zamani lilikuwa moto kweli kweli kwenye runinga moja kwa moja. Nina uamuzi mkubwa sana wa kuufanya… Bado naweza kumuamini kweli Grand P?” aliuliza mwanamitindo huyo.
Pendekezo hili la ndoa linamuweka Yao kwenye njia panda ashindwe la kuamua kama anaweza bado kumuamini mpenzi huyo wake wa zamani haswa baada ya kumuacha mwezi mmoja uliopita kwa kile alisema kwamba mwanamuziki huyo anatoka sana na wanawake tofauti tofauti na wiki chache baadae akamuona kwenye video akiogolea na mwanamke mwingine ambapo alimtakia kila la kheri katika kuyamumunya maisha kwa kijiko cha dhahabu.