logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msanii Ed Sheeran ashinda kesi ya hakimiliki kuhusu wimbo wa Shape of You

Sheeran alisema hakumbuki akisikia 'Oh Why' kabla ya kesi

image

Burudani06 April 2022 - 13:37

Muhtasari


  • Msanii Ed Sheeran ashinda kesi ya hakimiliki kuhusu wimbo wa Shape of You

Ed Sheeran ameshinda kesi kwenye mahakama ya juu zaidi juu ya hakimiliki ya wimbo wake wa mwaka 2017 uliovuma kwa jina-Shape of You.

Jaji aliamua Jumatano kwamba mwimbaji na mwandishi huyo hakunakili wimbo huo wa mwaka 2015 unaojulikana kama Oh Why ulioimbwa na Sami Chokri.

Chokri, ambaye ni msanii anayeimba chini ya nembo ya jina Sami Switch, alikuwa amedai kuwa "Oh I" ulijitokeza katika wimbo wa Sheeran "ukiwa unafanana sana" na wimbo wa "Oh why" ambao aliuimba mwenyewe.

Sheeran alisema hakumbuki akisikia 'Oh Why' kabla ya kesi

Shape of You ulikuwa ni wimbo uliouzwa zaidi nchini Uingereza mwaka 2017 na ni wimbo uliochezwa zaidi katika App ya Spotify kuwahi kushuhudiwa.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved