logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Mimi sitaki kuomba pesa" Nyota Ndogo aomba kukutana na Gavana Samboja

Nyota Ndogo amesema ana ujumbe muhimu wa kumpa Samboja.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri27 April 2022 - 10:41

Muhtasari


•Nyota Ndogo amesema amekuwa akifanya juhudi kubwa ikiwemo kujaribu kumfikia gavana huyo kwa  simu ila bado hajaweza kufua dafu.

•Ameomba walio na uwezo kumsaidia kufikia mwanasiasa huyo huku akisema ana ujumbe muhimu wa kumpa

Mwanamuziki Mwanaisha Abdalla almaarufu Nyota Ndogo amesema kwa muda sasa amekuwa akijaribu kukutana na gavana wa Taita Taveta Granton Samboja bila mafanikio.

Nyota Ndogo amesema amekuwa akifanya juhudi kubwa ikiwemo kujaribu kumfikia gavana huyo kwa  simu ila bado hajaweza kufua dafu.

"Watu wangu hivi mimi kweli mtu wakutafuta gavana samboja kweli? Lakini enyewe mimi ni nani kusema kweli?Naomba tu.Nimemtafuta na hata kuna majirani zangu wanaweza kunipeleka kwake lakini hata simu hupokelewi.Labda mtu anaweza ona hii akampa screenshot. Akamwambia pigia Nyota ama namna gani?" Nyota Ndogo amesema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mama huyo wa watoto wawili ameomba walio na uwezo kumsaidia kufikia mwanasiasa huyo huku akisema ana ujumbe muhimu wa kumpa. 

"Mimi sitaki kuomba pesa nipo na kibandiski town am ok nataka tu kuongea nae kidogo," Amesema.

Mwanamuziki huyo ambaye alipata umaarufu zaidi ya miongo miwili iliyopita ni mzaliwa wa eneo la Pwani. 

Kwa sasa hahusiki sana katika muziki bali anashughulika zaidi na mkahawa wake ulio katika katika eneo la Voi.

Takriban miezi miwili iliyopita mwanamuziki huyo alimwalika kinara wa ODM Raila Odinga katika hoteli yake wakati wa ziara yake katika kaunti ya Taita Taveta.

"Naskia Baba anakuja Voi. Aki wamlete hapa hotelini kwangu akule chakula ya Nyota Ndogo Jikoni. Nimuambie mawili matatu kuhusu bei ya chakula inavyotukandamiza. Endapo atachukua kiti basi aangalie Wakenya. Kura yangu siri yangu, ata Ruto alinipokonya tu. Swali ni, ataweza kula kibandani Baba?"Aliandika.

Mwaka jana  pia alikuwa amemualika naibu rais William Ruto wakati wa ziara yake katika kaunti ya Taita Taveta ila ombi lake halikutimia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved