logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bahati: Lengo langu ni kupata watoto 10, siwezi fanya vasektomia

“Kwa kweli wacha niseme mimi kwa upande wangu sina tatizo hata, lengo langu ni kuwa na watoto kumi. Najua Mungu atatubariki na nyumba kubwa ya kuweka hiyo familia yote,” Bahati alimwambia Diana Marua.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri28 July 2022 - 07:21

Muhtasari


• Kwa sasa, Bahati na Diana wana jumla ya watoto watano, pamoaj na huyo mtarajiwa.

Msanii Bahati Kioko na mkewe Diana Marua katika moja ya video yao YouTube

Mwanamuziki na mkuza maudhui wa YouTube, Diana Marua kwa siku kadhaa sasa amekuwa akizua mjadala mitandaoni akimtaka mumewe msanii na mwanasiasa Bahati Kioko kufanya vasektomia ili kujifunga kutomzalisha watoto wengine tena.

Katika video ambayo Marua alipakia kwenye YouTube yake Jumatano, alimtaka kwa msisitizo mkubwa Bahati kufunga mishipa ya uume wake almaarufu vasektomia kama njia moja ya kupanga uzazi kwa kile alisema kwamba hahitaji tena kubeba ujauzito mwingine baada ya ule ambao ako nao sasa hivi kwani huwa anapitia mateso sana pindi anapokuwa mjamzito.

Kwa upande wake, msanii Bahati Kioko alionekana akipinga vikali suala hilo la kufanya vasektomia huku akisema kwamba suala la upngangaji uzazi aghalabu linafaa kufanywa na wanawake.

Bahati alisema kwamba hayuko tayari kabisa kwa kuendea mchakato wa vasektomia kwani bado lengo lake ni kupata watoto kumi na ndio mwanzo amefika katikati ya lengo lake kwani sasa anaenda kuwa na mtoto wa tano katika familia yake kwa jumla, watatu wakiwa wale amezaa na Diana Marua, mmoja amezaa na Yvette Obura na mwingine ambaye aliasili kutoka kituo cha watoto.

“Kwa kweli wacha niseme mimi kwa upande wangu sina tatizo hata, lengo langu ni kuwa na watoto kumi. Najua Mungu atatubariki na nyumba kubwa ya kuweka hiyo familia yote,” Bahati alimwambia Diana Marua.

Jambo hili halikuonekana kuenda vizuri na Marua ambaye alisema yeye hayuko tayari kabisa kupata mtoto mwingine na hata huyu ambaye anamtarajia halikuwa jambo lililopangwa bali lilitokea ghafla tu kama chafya na kwa vile tayari yalishapwaa basi hakuwa na budi bali kuyapokea.

Juzi, Diana Marua alidokeza kwamba mimba hii anayoibeba inampa wasiwasi na mashaka makubwa ya woga kwani anaogopa tena kuenda kupitia mchakato wa kujifungua kwa mara nyingine, hata kama ako na hamu na furaha ya kumpokea mtoto wake wa tatu lakini ni suala ambalo linampa woga mkubwa na ndio maana anamtaka Bahati kufanyiwa mpango wa uzazi kwa njia ya vasektomia ili kuzuia suala kaam hilo la mimba ya ghafla kutokea tena siku za mbeleni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved