logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Unamtumia mume wangu picha chafu na meseji, tunazitazama pamoja na kukucheka" - Lady Risper

“Nina nywila za mume wangu za akaunti yake ya instagram na kila unapomtumia meseji zako za mapenzi na uchi, tunaangalia pamoja na kukucheka,” Lady Risper aliandika.

image
na Radio Jambo

Habari28 July 2022 - 08:38

Muhtasari


• Wengine walimtaka asijione ameshinda mchezo huo sana kwani huenda mumewe baadae anaenda kuwatafuta wanadada wale.

Mwanasosholaiti Lady Risper na mumewe Brayo

Mwanasosholaiti aliyestaafu Lady Risper amesema kwamba kuna wanadada ambao kutwa kucha wanamtumia mumewe picha za utupu kwenye kijisanduku faragha cha akaunti yake ya Instagram na kufichua kwamba ako na nywila za kuingia kwenye akaunti hiyo.

Risper alisema kwamba kila mara akiingia na kupata picha hizo chafu basi huwa wanazitazama pamoja na mumewe na kumcheka yule mwanadada ambaye hachoki kuzituma kwa lengo la kumyakua mumewe kutoka kwake.

“Nina nywila za mume wangu za akaunti yake ya instagram na kila unapomtumia meseji zako za mapenzi na uchi, tunaangalia pamoja na kukucheka,” Lady Risper aliandika.

Mama huyo wa watoto wawili alisema kwamab wapo wanawake wengi tu huku  nje wanaomtamani na kumtolea macho mume wake wakimtongoza kupitia DM  za akaunti zake za mitandaoni, lakini amewaambia serikali iko imara kwani yeye ana nywila za akaunti za mume wake na kila mara wanapoona jumbe za mapenzi na picha za utupu basi huwa wanamcheka aliyetuma.

Ufichuzi huu wa Lady Risper uliwashangaza wengi huku baadhi wakishangaa kwamba kuna wanawake ambao bado mpaka karne hii wanajidhalilisha kwa kutuma picha zao za utupu kwa mwanaume, bila hata mwanaume huyo kuomba atumiwe.

“Kama kuna wanawake huko ambao wanachagua kupeleka uchi zao kwa Brayo? Wanahitaji kuwa serious,” mmoja kwa jina Abby Nally alisema.

Wengine walimtania kwamba baada ya kumaliza kucheka pamoja pengine mumewe huenda kufanya uchunguzi wa chini ya zulia kuwatafuta, na hivyo kumtaka asijitie mikogo sana.

“Na baada ya kumaliza kucheka pamoja anawafuata na sasa wasichana hao wanakucheka wewe sana...wanaume watakuaibisha,” mwingine kwa jina Nanish Flora alimwambia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved