logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Felicity Shiru ajibu mashabiki walioulizia logbook ya gari alilopewa na Pluto

Felicity alizawadiwa gari hilo bila kutarajia kwenye sherehe yake ya uja uzito wake

image
na Radio Jambo

Habari27 September 2022 - 04:47

Muhtasari


•Felicity aliweka wazi kuwa Pluto alikuwa akimpa vidokezo vya kutaka kumzawadi gari ila hakutarajia kabisa kuwa itawahi kufanyika.

MwanaYouTube Felicity Shiru amejibu madai ya  baadhi ya wanamitandao kuhusu gari alilozawadiwa na mpenzi wake Robert Ndegwa alimaarufu Thee Pluto.

Felicity alizawadiwa gari hilo bila kutarajia katika hafla ya kumpongeza kwa kuwa kupata ujauzito. Alisema kwamba hakutarajia kuzawadiwa gari siku hiyo na hangeweza kuitisha stakabadhi za usajili wa gari hilo ila tu kumshukuru Pluto kwa  zawadi hiyo.

“Sasa ningeanza kumwambia Pluto anipe logbook ya gari? Eti  ndio niamini gari ni langu? Sasa karatasi zilikuwa ziendewe wapi?”alisema.

Aliwashauri watu kujifunza kushukuru wanachopewa kitu au kuzawadiwa na kutobagua zawadi wanazotaka kupewa na baadaye akamshukuru mpenzi wake kwa hafla.

“Asante sana Pluto kwa kupanga yote haya kwa ajili yangu, hakuna kitu nimefanya ama kuchangia. Kila kitu kilikuwa shwari ikiwemo chakula, MC na hata burudani. Na pia kwa zawadi uliyonipa leo,sikuwa nimetarajia,”alisema.

Felicity aliweka wazi kuwa Pluto alikuwa akimpa vidokezo vya kutaka kumzawadi gari ila hakutarajia kabisa kuwa itawahi kufanyika.

Wawili hao walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wa kike ingawa Felicity alikuwa akitarajia mtoto wa kiume baada ya kuambiwa na kupata maoni ya watu akiwemo mama yake kuwa uja uzito wake ni wa kiume.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved