logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtoto wangu ananyonya mpaka ziwa analiacha mwenyewe - Nandy ajibu wanaouliza mtoto

Alisema maisha yake ya mitandaoni na ya uhalisia ni pande mbili tofuati za sarafu .

image
na Radio Jambo

Habari31 December 2022 - 11:14

Muhtasari


• Msanii huyo alisema awali kuwa hakuwa na mpango wowote wa kumuonesha mwanawe kwenye mitandao ya kijamii mpaka pale atakapokuwa mkubwa.

• Watu wamekuwa wakizua mitandaoni kuwa huenda hana mtoto na anadanganya jambo ambalo limemfanya kuwajibu vikali.

Nandy

Msanii Faustina Charles almaarufu Nandy kutoka Bongo amewacharukia baadhi ya mashabiki wake ambao kila mara wanamganda kama ruba kisa kutaka kujua hali ya mtoto wake na Billnass.

Msanii huyo katika ujumbe mrefu ambao aliuandika Instagram alionekana kuchukia maswali kama hayo huku akiwaambia mashabiki zake kukoma kuchokonoa mambo ya kifamilia bali wabaki tu kwenye mstari wao wa kuwa mashabiki na kusapoti kazi za Sanaa tu basi.

Nandy alisema kuwa si mara ya kwanza anaulizwa iwapo mtoto wake anafurahia ukaribu wake na kunyonya saa ngapi kutokana na mishe zake nyingi ambapo hajawahi onekana hata mara moja na mwanawe.

Aliwatoa wasiwasi kwa kujibu kuwa mtoto wake ako naye muda mwingi tu kila anapoenda sema hajataka kumuonesha hadharani kwa mapaparazi na wapiga picha. Alisema kuwa mwanawe anafurahia kampano yake muda wote na anafurahia maziwa ya mama mpaka ziwa analiacha mwenyewe.

“Hili swala kila nikipost watu wanauliza mtoto yuko wapi? Mara mtoto ananyonya saa ngapi? Jamani hivi mnahisi mambo ya familia ni maigizo au nimezaa fasheni? Mtoto wangu nipo naye kila muda na anapata malezi yote kwa wazazi kama watoto wengine kwa wazazi wao,” Nandy alifoka.

Aliwataka mashabiki zake kuona utofauti kati ya maisha ya uhalisia na yale ya mitandaoni huku akisema kuwa wakianza kufuatilia maisha ya mitandaoni na kufikiri ni ya uhalisia, basi watakuwa hata robo ya maisha yake hawajayajua.

“Msichanganye maisha ya Insta na maisha ya ndoa na yale ya Uhalisia. Huku Insta maisha yangu hata robo hayajafika. Popote nilipo na mtoto wangu yupo, ananyonya mpaka anakataa ziwa mwenyewe, ansshinda na mimi mpaka nikitokea anasikia sauti anaruka kama kichaa. Tuendelee kusapoti muziki mambo ya kifamilia achene niyafurahie faraghani,” Nandy alisema.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved