logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Wewe ni kama baba yangu, huwezi kunioa" - Linet Toto amjibu mzee aliyemmezea mate

Alisema kuna mzee kwa jina Kirwa aliyependekeza kufunga ndoa naye.

image
na Davis Ojiambo

Burudani12 February 2023 - 11:02

Muhtasari


  • • Toto alimtaka mzee huyo kumtafutia mwanamume wa rika lake na si kutaka kumuoa yeye.
Linet Toto amkataa Kirwa

Jumamosi mbunge wa Mogotio, Reuben Kiborek alikuwa na hafla katika eneobunge lake akitoa shukrani kwa wananchi kumchafua katika uchaguzi wa Agosti mwaka jana.

Hafla hiyo ilifanyika katika eneobunge hilo na ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka eneo pana la Bonde la Ufa akiwemo mwakilishi wa kike wa kaunti ya Bomet Linet Chepkorir almaarufu Toto.

Mbunge huyo wa kaunti ya Bomet aliyegonga vichwa vya habari kwa kuwa mchanga Zaidi kuwahi kushinda uchaguzi mwaka jana aliwachekesha wengi alipokataa ombi la mzee mmoja aliyetaka kumuoa.

Toto alisema kuwa mzee huyo kwa jina Kirwa aliyeonesha nia ya kutaka kumfanay kuwa mke wake alikuwa mkubwa Zaidi kiumri kumliko huku akisema kuwa jambo kama hilo haliwezekani kwani yeye ni kama mjukuu wake.

Toto alimtaka mzee huyo badala ya kutaka kumuoa, amtafutie mwanamume mwingine mwenye rika lake ili wakaoane, kwani alikuwa na nia ya kupata mwanamume mzuri na wala sim zee wa rika la babu yake.

“Mmemsikia Kirwa akisema anataka kunioa. Wewe ni kama baba yangu, huwezi kunioa. Nitafutie mchumba ambaye ni mwenza wa umri wangu. Nahitaji aliye katika rika langu," alisema huku umati ukiangua kicheko.

Kando na Toto, wengine pia waliohudhuria ni waziri wa usafiri na miundombinu wakili Murkomen ambaye alishangazwa kwamba familia nyingi katika kaunti ya Baringo zilikuwa zinapitia ukame na ugumu wa njaa.

Alimzawidi Kiborek taslimu ya nusu milioni na kumtaka kuzitumia kuwasaidia watoto maskini kila familia kwa angalau kiasi cha kati ya elfu 20 hadi 30.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved