logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Esther Musila: Sina nguvu ya kuchukia mtu yeyote, ni kuwaombea tu mpone hiyo chuki!

"Ukinichukia ni ama nikuombee upone, nikupende au nikutakie mema,” Musila alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani13 March 2023 - 05:51

Muhtasari


  • • Musila amemuacha Angel kwa takribani miaka 20 na hilo limekuwa likiibuliwa kama gumzo la kigezo cha umri katika ndoa baina ya mume na mke kila mara.
Estehr Musila asema hana chuki dhidi ya wanaomchukia.

Esther Musila, mke wa mwanamuziki wa injili Guardian Angel amefichua kwamba chuki ya watu mitandaoni dhidi yake wala haikoseshi usingizi hata kidogo kwenye maisha yake. Chuki na kejeli mitandaoni pia alisema hazijawahi zua mkwamo wowote katika ndoa yake na msanii Guardian Angel.

Musila aliweka wazi kwamba wale wote wanaoendeleza chuki na kejeli dhidi yake wanafanya kazi bure kwani hawamkomoi hata chembe.

Mama huyo wa watoto watatu alisema kwamba katika maisha yake, hana nguvu wala uwezo hata kidogo kwenye nafsi yake kulipiza chuki kwa chuki, na hio halijawahi muingia akilini hata kidogo.

Dawa ya wenye chuki kulingana na Musila, ni kuwapenda, kuwatakia mema au kuwaombea wapone kutokana na chuki hiyo.

“Sina nguvu hata kidogo nafsini mwangu kumchukia mtu yeyote. Kiuhalisia sina nafasi hiyo katika moyo wangu. Ukinichukia ni ama nikuombee upone, nikupende au nikutakie mema,” Musila alisema.

Musila na mumewe Guardian Angel wamekuwa wakikejeliwa mitandaoni kwa ndoa yao kutokana na utofauti mkubwa uliopo baina ya umri wao.

Musila amemuacha Angel kwa takribani miaka 20 na hilo limekuwa likiibuliwa kama gumzo la kigezo cha umri katika ndoa baina ya mume na mke kila mara, Zaidi ya mwaka mmoja tangu wawili hao kuwa mwili mmoja katika hafla ya faraghani.

Wikendi iliyopita, Musila alifichua kwamba licha ya watu wengi kumshambulia hadharani kutokana na umri wake mkubwa, lakini mamia ya watu hao hao ndio aghalabu hufurika kwenye faragha za kurasa zake mitandaoni wakitupa ndoana kwa moyo wake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved