Bahati na Diana B waenda likizo ughaibuni

Wawili hao waliabiri ndege JKIA.

Muhtasari

•Bahati alidai kuwa Diana alilalamika kuwa hakumfanyia lolote siku ya akina mama duniani hivyo basi aliamua kupeleka likizoni.

Msanii Bahati na mkewe Diana B siku ya Jumatatu walifunga safari kuelekea kwenye likizo ughaibuni.

Kwenye mtandao wa Instagram, Bahati na Diana walionekana  wakiabiri ndege  katika uwanja wa ndege wa JKIA. Wawili hao walijiburudisha kwa vyakula vya kumezewa mate na kulishana mahaba si haba.Waliipamba kuondoka kwao kwa kuvaa nguo zinazolingana.

 

Bahati na Diana walisema kuwa  siku zijazo wakiwa kwenye likizo ndizo zitakuwa siku bora zaidi kwa kumbukumbu, pia aliuliza mashabiki ni kipi atamfanyia Diana B ili iwe kumbukumbu bora zaidi kwake.

"Mpenzi, siku chache zinazofuata zitakuwa bora zaidi kiliko ambazo umekuwa nazo,kumbukumbu, Nimfanyie nini mrembo huyu ili iwe likizo bora zaidi?" Bahati aliuliza.

 

Bahati alidai kuwa Diana alilalamika kuwa hakumfanyia lolote siku ya akina mama duniani hivyo basi aliamua kumpeleka likizoni.Ingawa hakusema ni wapi wanakokwenda,walionekana kwenye sehemu ya ndege za Turkish Airlines.

"Malkia wangu alilalamika kuwa sikumfanyia lolote siku ya wanawake," alisema Bahahati.Aliongeza kwa kuuliza kama watu wanajua wanakoenda

Diana B kwenye mtandao wa Instagram aliuliza ni kwa nini Bahati hakumweka mtandaoni siku ya wanawake duniani.

"Bahati kwanini hukunipost siku ya wanawake duniani?" Diana alichapisha

Diana alifurahia safari yake na Diana mtandaoni,

"Kusafiri duniani na mpenzi wangu Bahati,' Diana alisema.

Diana B hivi majuzi amekuwa na ugomvi mtandoni baada ya kudai kuwa Andrew Kibe anatusi watu mtandaoni ilhali yeye ni masikini.Andrew Kibe kwa upande wake alijibu akisema kuwa Diana hajaona gari lake alilonunua  hapo awali.