logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Betty Kyallo adokeza kupata mtoto wa pili hivi karibuni, "Binti yangu anahitaji ndugu!"

Kyallo ana binti mmoja ambaye walizaa na mwanahabari Dennis Okari kabla ya kuachana.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri16 March 2023 - 05:50

Muhtasari


• Pia, Kyallo alidokeza mipango ya kufungua miradi mingine katika wiki ya pili ya mwezi Aprili.

• Alisema hawezi igiza katika filamu ya Real Housewives of Nairobi kwa kile alisema ina mambo mengi mabaya na yeye anapenda maisha mazuri.

Betty Kyallo kupata mtoto wa pili hivi karibuni.

Mwanahabari wa muda mrefu kwenye runinga, Betty Kyallo ambaye sasa hivi ni mjasiriamali katika sekta ya huduma za saluni na kinyozi amedokeza kwamba ni wakati sasa anahitaji kupata mtoto wa pili.

Kyallo ambaye alikuwa anazungumza na wanablogu katika uzinduzi wa maeneo mapya ambako alihamishia biashara yake ya saluni na Kinyozi kwa jina Flair by Betty, alisema kwamba mtoto wake wa kwanza ambaye walizaa na mwanahabari mwenza Dennis Okari kabla ya kutengana amekuwa akimpa shinikizo la kutaka ndugu.

Mwanahabari huyo alisema kwamba atang’ang’ana safari hii na kupunguza shinikizo hilo kwa kumzalia kifungua mimba wake ndugu.

“Kusema kweli ndio, nafikiri ni muda wa kufikiria kuongeza familia, mtoto. Ivana amekuwa akinipa shinikizo la kutaka dada, kaka. Nafikiri anahitaji mtu wa kumpa ushirikiano, nitamtafutia, nitang’ang’ana,” Kyallo alisema kwa furaha.

Awali, mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor ambaye alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliofika kuhudhuria uzinduzi huo mpya aliwatania wanablogu kwamba angewaonesha sehemu alikokuwa ameketi mpenzi mpya wa Betty Kyallo, akisema kwamab yuko na anamjua lakini hakuwa amekaribia sehemu alikokuwa Betty.

Kwa upande wake, Kyallo alisema kwamba ukimya wake kutoka kwenye mtandao wa YouTube haswa kufanya video mbali mbali hatimaye huenda ukamalizika hivi karibuni. Alisema kuwa tayari amepata maudhui mengi ambayo atawamegea wafuasi wake sugu kwenye mtandao huo wa video.

“YouTube nitarudi, nafikiri sasa hivi nimepata maudhui, angalau sasa hivi niko na kitu cha kiambia watu, sit u kwa sababu niko na YouTube nikuwe tu napakia vitu visivyofurahisha masahbiki wangu,” Kyallo alisema.

Mjasiriamali huyo alifichua kwamba katika wiki ya pili ya mwezi Aprili, atazindua tena biashara nyingine ambayo hata hivyo hakuizungumzia kwa undani.

Kuhusu filamu mpya amayo inazidi kutamba kwa jina ‘Real Housewives of Nairobi’ Kyallo alisema tayari ameifuatilia lakini akasema kwamba hangependa hata kidogo kuigiza katika filamu hiyo.

Alisema kwamba filamu hiyo iko na mambo mengi ambayo kwake hawezi kuyafanya kutokana na kujikubali na maisha yake yaliyolainika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved