logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa nini Kim Kardashian anataka kustaafu usosholaiti na kuwa wakili na mwanaharakati?

Kazi ya mageuzi ya Kim ilianza Oktoba 2017 baada ya kujifunza kuhusu kesi ya dada aliyefungwa kwa dawa za kulevya.

image
na Davis Ojiambo

Burudani01 May 2023 - 09:10

Muhtasari


  • • "Kila mara mimi hutania mama yangu - ambaye ni meneja wangu - nasema Kim K. anastaafu, na mimi nitakuwa tu wakili." - Kim alisema.
  • • Kazi ya mageuzi ya Kim ilianza Oktoba 2017 baada ya kujifunza kuhusu kesi ya dada mmoja aliyekuwa gerezani tangu Oktoba 1996.
Kim Kardashian atathmini kuacha usosholaiti na kuwa wakili.

Mashabiki wake kote ulimwenguni hawawezi kufikiria showbiz bila Kim Kardashian lakini nyota huyo wa vipindi vya uhalisia kwenye runinga hakika anaweza.

 Kim hivi majuzi alifichua mustakabali wake katika vuguvugu la mageuzi ya haki ya jinai alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano wa TIME100.

Kim alidokeza kwamba anatathmnini kuachia mbali kufanya vipindi vya uhalisia kwenye TV na kujitupa muda wote katika masuala ya kisheria.

"Ningefurahi vile vile kuwa wakili wakati wote," alijibu alipoulizwa ikiwa angewahi kufikiria maisha bila kutazamwa runingani. "Safari hiyo ilinifungua macho sana," alishiriki, na kuongeza, "Inakuwa nzito kwa sababu kuna mengi ya kufanywa ... nilimleta dada yangu Khloe (Kardashian) gerezani kwa mara ya kwanza wiki iliyopita, na hilo lilimfungua macho sana.”

Kim Kardashian bado si mwanasheria rasmi lakini nyota ya Keeping Up With The Kardashian alimwambia mtangazaji Poppy Harlow kwamba anatumai kuwa juhudi zake katika harakati za kisheria zitakuwa "kazi yake ya maana zaidi maishani."

"Natumai hivyo," alisema, na kuongeza, "Kila mara mimi hutania mama yangu - ambaye ni meneja wangu - nasema Kim K. anastaafu, na mimi nitakuwa tu wakili."

Kazi ya mageuzi ya Kim ilianza Oktoba 2017 baada ya kujifunza kuhusu kesi ya Alice Marie Johnson, ambaye alikuwa gerezani tangu Oktoba 1996 baada ya kuhukumiwa kwa kusaidia kuwezesha mawasiliano katika kesi ya biashara ya madawa ya kulevya.

Alijitolea wakati wake kumwachilia Johnson na hata alikutana na Rais wa zamani Donald Trump juu ya suala hilo. Trump alibadili hukumu yake mwaka wa 2018 na Johnson akaachiliwa.

Tangu wakati huo, Kim ameendelea kutetea kuachiliwa kwa wafungwa wengine kadhaa na akafichua mnamo 2019 kwamba alikuwa akisomea kuwa wakili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved