Kwa mara nyingine tena msanii Chris Brown amejikuta kwenye sakata la mapigano baada ya kudaiwa kupigana na mwenzake Usher Raymond.
Mambo yanasemekana kupamba moto kati ya Usher na Chris Brown kwenye tafrija ya hivi majuzi ambapo walibishana kabla ya Brown kudaiwa kumrukia Usher kama nyoka wa kifutu na kumuacha akilowa damu.
Mastaa hao wa Marekani wote walikuwa kwenye ukumbi wa Skate Rock City mjini Las Vegas, ambapo Chris alikuwa akisherehekea miaka 34 ya kuzaliwa kwake, jarida la Metro linaripoti.
Walakini, picha za video zinaonyesha mwimbaji wa Loyal na mwimbaji wa OMG, 44, hawakumaliza usiku kwa masharti ya urafiki zaidi.
Kulingana na ripoti, Usher - jina kamili Usher Raymond IV - na marafiki zake waliimba siku ya kuzaliwa ya Chris mapema, lakini mambo baadaye yalikuwa mabaya.
Kama ilivyo kwa TMZ, walioshuhudia walimwona Chris akijaribu kuzungumza na Teyana Taylor, 32, alipokuwa ameketi kwenye benchi nje kidogo ya uwanja.
Lakini inaaminika, kwa sababu yoyote ile, alikuwa akimpuuza.
Kutokana na hali hiyo, Chris aliripotiwa kukerwa na kuanza kumzomea, ndipo rafiki wa muda mrefu Usher aliingilia kati kutuliza hali hiyo.
Hata hivyo, Chris inasemekana alianza kuwatukana Teyana na Usher, lakini alielekeza hasira zake nyingi kwa Usher.
Hatimaye, Chris na wafanyakazi wake walikuwa wakiondoka, wakati ambapo kundi hilo linaaminika kuwa lilitoka nje ya ukumbi huo.
Usher na Chris wamekuwa marafiki kwa miaka kadhaa.
Licha ya kuwa mara nyingi wanazozana katika ulimwengu wa muziki, wameendelea kuwa karibu na mara nyingi waliweka wazi kuwa ushindani wa chati hauwasumbui.
Kwa kweli, mnamo 2020, Chris alienda kwenye Instagram kuonyesha zawadi ya Krismasi aliyopokea kutoka kwa Usher - ambayo ilikuwa pikipiki.