logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jimal amshtumu aliyekuwa Amira kwa kudai kuwa saa yake ni bandia

Jimal Roho safi amemshtumu aliyekuwa mkewe Amira kwa kudai kuwa saa yake ni bandia.

image
na

Yanayojiri11 May 2023 - 05:59

Muhtasari


• Jimal alisema kua saa yake si bandia na ilimgharimu shilingi milioni 2.3.

• “Si aninunulie saa asili basi kwa maana ni yeye anayezijua saa bandia na asili”

Jimal Rohosafi na aliyekuwa mke wake Amira

Mwanasosholaiti Jimal Rohosafi ambaye pia ndie mwenyekiti wa wamiliki wa matatu mjini Nairobi amemshtumu aliyekuwa mkewe Amira kwa kudai kuwa saa yake ni bandia.

Akizungumza na kituo kimoja cha radio nchini, Jimal alisema kwamba saa yake si bandia na ilimgharimu shilingi milioni 2.3. Jimal alijibu madai haya baada ya mashabiki wake kuibua tetetsi kuwa saa ile ilikuwa bandia.

“Saa yangu ni asili, nimeinunua shilingi milioni 2.3, kwanza si mimi nilinunua nilipewa kama zawadi na rafiki yangu anayekaa Dubai.” Jimal alisema.

Jimal aliongeza kuwa kama Amira alihisi kuwa saa yake ilikua bandia angemnunulia saa asili kwa maana alikua anajiskia kuwa na hela mingi.

“Si aninunulie saa asili basi kwa maana ni yeye anayezijua saa bandia na asili”

Jimal na Amira walikua wana ndoa na waliachana baada ya Jimal kuchumbiana na mwanasosholaiti mwingine  Amber Ray.

Jimal alimhakikishia Ankali Ray kuwa hawezi akamrudia mke wake wa zamani.

“Mimi huyo sitamsikiza , sitaki kumfanya awe maarufu na sitamwongelelea tena kwa kuwa yeye ni mtu mdogo sana kwangu.” Aliongeza Jimal.

Aliongeza kuwa mke wake mpya Wangari yuko salama baada ya kuondoka hospitalini alikokuwa kwa siku 14 akiiguza mwanao mchanga.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved