Wimbi la janga la Covid-19 linazidi kuwasakama mastaa wengi wa Bongo ambapo sasa msanii Zuchu amekuwa wa hivi karibuni kutangaza anaugua ugonjwa huo.
Malkia huyo wa WCB Wasafi kupitia akaunti yake ya Snapchat alidokeza kwamba amekuwa mtu wa hivi punde kuingia kwenye msururu wa kutekwa na Corona.
Zuchu ambaye alikuwa anatarajiwa kuachia remix ya ngoma yake ya ‘Nani’ na msanii kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Innos B alilalamika kwamba gonjwa hilo linamkwamisha pakubwa katika mambo yake na kulitaka limpe uhuru na Amani yake.
“Corona niachie huru tafadhali,” Zuchu aliandika huku akiweka emoji za kukasirika na kulia.
Msanii huyo anatangaza kushambuliwa na virusi hivyo wiki moja tu baada ya mwigizaji Kajala Masanja pia kudokeza kwamab alikuwa anaugua kutokana na wimbi hilo lakini pia anayedhaniwa kuwa mkaza mwana wake, msanii Marioo pia alisemekana kuugua Corona.
Binti wa Kajala, Paula Kajala naye pia alidokeza kuwa ni kweli wala sio kiki kama ambavyo wengi walikuwa wakifikiria akiwaandikia Mpenzi wake Marioo na mama yake Kajala ujumbe wa kuwatakia afueni ya haraka.
Hata hivyo, katika miaka kama miwili hivi iliyopita, gonjwa la Corona halijakuwa kitu cha kukeketa sana kama ambavyo iikuwa mwaka 2020 mapema ugonjwa huo ulipozuka kote duniani.