logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kanye West anachukia watu weusi licha ya kwamba yeye ni mweusi pia - rapa Boosie Badazz

Boosie alidai kuwa Kanye anatumia jukwaa lake kubomoa na kuwadhalilisha watu Weusi.

image
na Davis Ojiambo

Burudani15 June 2023 - 05:03

Muhtasari


  • • Boosie Badazz kisha akachukua msimamo mkali, akisema kwamba maneno ya Kanye West, haswa kwa George Floyd mnamo 2022 yalikuwa na madhara kwa watu weusi

Katika mahojiano ya hivi majuzi na YouTube Math Hoffa kwenye kipindi cha “My Expert Opinion”, rapa wa Marekani, Boosie Badazz alieleza kusikitishwa kwake na rapa mwenzake Kanye West na kumshutumu kuwa hana mapenzi wala heshima kwa watu za Weusi.

Boosie alidai kuwa Kanye anatumia jukwaa lake kubomoa na kuwadhalilisha watu Weusi licha ya kuwa yeye pia ni mtu mweusi.

Ukosoaji huo unakuja kutokana na maoni tata ya Kanye katika siku za nyuma, ikiwa ni pamoja na madai yake kwamba utumwa ulikuwa chaguo na kupendekeza kwamba George Floyd alikufa kutokana na fentanyl – dawa za kupunguza uchungu - na sio Derek Chauvin.

Boosie anaamini kwamba hakuna mtu aliyezaliwa huru anayeweza kuelewa utumwa na kuongeza kuwa kama angezaliwa huko Kusini mwa Antebellum, labda angekuwa mtumwa.

"Nilichukizwa na Kanye West," Boosie Badazz alisema. "Nilichukizwa na Kanye. Nilikuwa nikitweet kuhusu yeye na kila kitu. Nilikuwa nikiandika maneno mabaya. Sipendi chenye Kanye anafanya kwa watu wote Weusi. Sijui Weusi walimfanyia nini. Ninahisi kama Kanye West hapendi watu Weusi.”

Mazungumzo hayo yalibadilika haraka hadi kwa maoni ya Ye kutoka 2018 aliposema kwamba "utumwa ulikuwa chaguo." Wakati Maff Hoffa anaamini kuwa lilikuwa chaguo, Boosie Badazz anakanusha vikali msimamo huo.

"Ninahisi kama mtu, kutokana na kile nilichomwona akifanya na kuzungumza kuhusu watu Weusi, ninahisi kama hana upendo au heshima kwa jamii ya weusi," Boosie alielezea. "Ninahisi anapenda ngozi nyeupe zaidi."

Boosie Badazz kisha akachukua msimamo mkali, akisema kwamba maneno ya Kanye West, haswa kwa George Floyd mnamo 2022 yalikuwa na madhara kwa watu weusi kwa ujumla.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved