Mke wangu ni mtu anafanya zoezi ya kuwa mjane - Gaucho

"Hata juzi nimempa watu wenye wanaweza kumrithi wawili. Sasa yeye ndio atachagua kama kitu itatokea,” Gaucho alisema.

Muhtasari

• Mwanasiasa huyo alisema kuwa alifanya hivyo baada ya kiangalia na kugundua kuwa hakuna tofauti kati ya urafiki wa kazi ya ujambazi na kazi ya siasa.

Gaucho, rais wa Ghetto.
Gaucho, rais wa Ghetto.
Image: Screengrab//ObinnaTV.

Mwanaharakati na mwanasiasa Gaucho ambaye anafaamika sana kama rais wa Ghetto amesema kuwa maisha yake katika siasa ni yenye changamoto nyingi kiasi kwamba ameshamwandikia wosia mkewe wa kumpa wanaume wawili wa kuchagua mmoja wa kumrithi endapo mambo yatamwendea mrama.

Katika mahojiano na Oga Obinna, Gaucho alisema kuwa katika siku za hivi karibuni amekuwa mgeni wa seli kwenda na kurudi kiasi kwamba alihisi maisha yake yanawidnwa.

Alisema kuwa kutokana na kuhofia hivyo, alilazimika kumpa mkewe chaguo mbili za wanaume wa kusimama kama mrithi wake endapo atapatana na mkasa katika harakati zake za kutetea wanyonge.

“Niliambia mke wangu aniache kwa hii dunia ingine ya siasa juu hebu nikuulize, hii wiki imeisha nah ii ndio sijashikwa. Kila siku nakuwa kwa DCI mara nimechukuliwa kwa magari matano, nimeachiliwa. Sasa huyu ni mwanamke anafanya zoezi ya kuwa mjane. Hata juzi nimempa watu wenye wanaweza kumrithi wawili. Sasa yeye ndio atachagua kama kitu itatokea,” Gaucho alisema.

Mwanasiasa huyo alisema kuwa alifanya hivyo baada ya kiangalia na kugundua kuwa hakuna tofauti kati ya urafiki wa kazi ya ujambazi na kazi ya siasa.

“Unajua siasa iko na mambo mingi. Maisha ya ujambazi, unajua vizuri muda wowote unaweza ukapigwa. Vile vile hakuna pia mahali iko na uadui kama siasa, iko vita ya ndani, na pia kuna vita ya mshindani. Na ya ndani ndio kubwa kuliko ya mshindani juu huyu humuoni,” alisema.