logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ushauri wa Kamene Goro kwa warembo wanaotamani kutoka kimapenzi na Obinna

“Obinna anapenda mwanamke mwenye kichwa na fikira kama zake, kwa hiyo jifunze jinsi na kuwa na mzungumzo"

image
na Davis Ojiambo

Burudani27 June 2023 - 11:42

Muhtasari


  • • Pia aliwashauri warembo kufahamu kuwa kama Obinna ameshakuamini, hufai kuanza kumwekea ulinzi na kumfuatafuata nyuma kama una wasiwasi naye.
Kamene Goro awashauri vidosho jinsi ya kumpata Obinna kimapenzi.

Kamene Goro ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa mchekeshaji Oga Obinna amewashauri vidosho wanaolilia ngoa penzi la Obinna jinsi ya kulipata penzi hilo na kubwa Zaidi jinsi ya kuhakikisha kwamba penzi na Obinna linadumu.

Kwa mujibu wa Kamene, Obinna ni mtu mmoja ambaye huwahukumu warembo na kuwasoma tabia zao kutokana na maongezi yao.

Kamene alisema kuwa katika kipindi ambacho wamekuwa marafiki na Obinna, anafahamu fika kwamba mchekeshaji huyo ana pesa lakini hapendi warembo ambao ni wa kuongea kila mara, huku pia akiwashauri kutoweka ombi la pesa kutoka kwa Obinna iwapo wanataka wachumbiane naye, kwani atawapa tu mwenyewe bila kuombwa.

“Kitu kimoja ambacho mnafaa kujua, Obinna ni mtu ambaye atakuhukumu kutokana na maongezi yako. Kama wewe ni dem wa kuzungumzia vitu kama sheesha, unaanza kumuomba pesa… nisikilize, Obinna ana pesa, atakupa pesa lakini usimuombe. Si eti uanze kujifanya, beb hiyo uber utanilipia. Acha kabisa,” Kamene alishauri.

Pia aliwashauri warembo kufahamu kuwa kama Obinna ameshakuamini, hufai kuanza kumwekea ulinzi na kumfuatafuata nyuma kama una wasiwasi naye.

“Obinna anapenda mwanamke mwenye kichwa na fikira kama zake, kwa hiyo jifunze jinsi na kuwa na mzungumzo, jua nini kinaendelea duniani, sio kila kitu kitakuwa kuhusu vilabu na usikunywe pombe ukajisahau, usivute sheesha, bangi au sigara, usiombe pesa, penda watoto halafu pia kuwa mpenzi mzuri, na usikuje kwake kama una kucha mbovu,” Kamene alitaja baadhi ya vitu ambavyo warembo wanaootamani kutoka kimapenzi na rafiki yake Obinna wanafaa kuzingatia.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved