Mrembo mmoja wa Nigeria kwa jina Chisom Flower ameomba msamaha hadharani baada ya awali kumkaripia msanii wa Afrobeats Davido akidai kwamba naye alikuwa na mimba yake.
Awali, mrembo huyo alifoka vikali kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa Davido aliwahi kumpa mimba ya hata kumpa Naira za Kinigeria milioni 10 ili kuavya mimba hiyo.
Mrembo huyo alikwenda hatua Zaidi kwa kupakia video ya mtu aliyedhaniwa kuwa Davido akiwa kwenye kitanda chake pamoja pia na ushahidi mwengine ulionuia kutia malalamishi yake nguvu na kuwaaminisha watu.
Mrembo huyo hata hivyo ameonekana kubadili msimamo wake baada ya kurudi kwenye mitandao ya kijamii na kumtaka Davido kumsamehe lakini pia akawaomba Wanigeria wote msamaha kwa kile alisema ni kutaka kumharibia msanii wao pendwa jina.
Alisema kwamab ameshapoteza kazi yak kutokana na tuhuma hizo na kumtaka ampe msamaha.
“Nimepoteza kazi yangu, familia na marafiki, hata chapa ninayofanyia kazi… Ninaomba radhi kwa David kwa kumkaripia hivyo na pia Wanigeria kwa kuvuta kipenzi chenu, naomba radhi.” Aliandika kwenye Instastory yake.
Chisom alijitokeza kusimulia kisa chake wakati Davido akiburuzwa mtandaoni na anayedaiwa kuwa ni mchepuko wake wa Marekani, Anita Brown na mchepuko wa pembeni wa Ufaransa, Ivanna, ambao wote walidai kuwa na ujauzito wake.