logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Obinna kusema ukweli nimepagawa na wewe - Brian Chira amwambia Obinna uso kwa uso!

Chira alimpongeza Obinna kwa muonekano wake baada ya kukutana ana kwa ana.

image
na Davis Ojiambo

Burudani05 July 2023 - 08:36

Muhtasari


  • • Baada ya kutamka kwamba anapagawa kwa Obinna, mchekeshaji huyo alimkatisha kwa haraka.
  • • Chira alisema kuwa kipindi hicho ndio mara ya kwanza alikuwa amefanya video akielezea ulimwengu kwamba alikuwa na anaishi na virusi vya UKIMWI.
Brian Chira akiri kupagawa na Obinna.

Mwanatiktok mwenye utata Brian Chira hatimaye amekutana na mchekeshaji Oga Obinna miezi kadhaa baada ya video yake kusambaa akilia huku akimwita Obinna.

 Katika mahojiano na mchekeshaji huyo kwenye chaneli yake ya YouTube, Obinna alimuuliza ni kwa nini alikuwa analia na kujigaragaza akiliita jina lake na Chira akaweka waziwazi kwamba alikuwa amepagawa na bado anapagawa na yeye.

“Kusema ukweli Obinna unakaa vizuri, nafikiri nilikuwa nimepagawa na wewe, na bado nahisi nimepagawa na wewe, kwa muktadha wa maudhi. Na ikiwa kuna mtu ambaye nilikuwa nataka anikuze na kunishika mkono katika sekta ya radio kwa sababu hiyo ndio kazi nataka, basi wewe ndio mtu wa kwanza ambaye ningependa,” Chira alisema.

Hata hivyo, baada ya kutamka kwamba anapagawa na Obinna, mchekeshaji huyo alimkatisha kwa haraka na kumtaka kukoma kusema hivyo la sivyo mahojiano hayo yatamatishwe mara moja.

Hapo ndipo Chira alieleza wazi kwamba si kupagawa ambako wengi wanaweza kufikiria bali ni kupagawa kwa muktadha wa ukuzaji maudhui.

Itakumbukwa hii si mara ya kwanza kwa tiktoker huyo kuibua madai tatanishi kuhusu suala la LGBTQ, kwani miezi kadhaa nyuma alifanya video kwenye TikTok yake akikiri mapenzi yake kwa mwanablogu Andrew Kibe ambapo alisema kuwa anapagawa na ndevu zake.

Chira alisema kuwa kipindi hicho ndio mara ya kwanza alikuwa amefanya video akielezea ulimwengu kwamba alikuwa anaugua virusi vya UKIMWI na alikuwa anapitia msongo wa mawazo kwa kufikiria jinsi watu watakuwa wanamchukulia na kumuona.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved