logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Amber Ray awadokezea mashabiki wake kuondoka Kenya kabisa

Amber Ray na mpenzi wake wamewadokezea mashabiki kuwa hivi karibuni wataondoka Kenya na kutafuta makazi nje ya nchi.

image
na

Grafiki25 July 2023 - 10:56

Muhtasari


• Amber Ray na mpenzi wake Kennedy Rapudo wamewadokezea mashabiki kuwa hivi karibuni wataondoka Kenya na kutafuta makazi nje ya nchi.

• Mwanabiashara huyo aliongeza kuwa sababu ya mahusiano yake na Amber Ray kudumu kwa muda mrefu ni kwa ababu ya rhema za Mungu na kutoiga mahusiano ya soshalaiti wengine.

Keneedy Rapudo ataja ufanisi wa ndoa yake na Amber Ray.

Amber Ray na mpenzi wake Kennedy Rapudo wamewadokezea mashabiki wao kuwa hivi karibuni huenda wakaondoka Kenya  na kuhamia kwingine. 

Wawili hao, wakizungumza na runinga ya mitandaoni ya SPM BUZZ wakati wa hafla ya kufahamu jinsia ya mtoto wa Eric Omondi, waliwaeleza wafuasi kuwa wanapanga kuondoka Kenya kabisa.

"Tumekuwa tukifikiria kwa sana na sioni tukiishi Kenya hivi karibuni. Tunapanga kuondoka na kuhamia nchi nyigine. Hamuezi jua tutaondoka na privat jet kwa sababu nafanya kazi kwa bidii na pia mke wangu anataka pirivate jet. so…"

Mfanyibiashara huyo aliongeza kuwa sababu ya mahusiano yake na Amber Ray kudumu kwa muda mrefu ni kwa sababu ya rehema za Mungu na kutoiga mahusiano ya soshalaiti wengine.

"La kwanza ni neema ya Mungu kwa sababu sisi tunaomba Mungu sana, na pia tunaishi maisha yetu vile tunajua na hatutafuata maisha ya watu wengin katika jamii."

Awali Rapudo aliwaeleza mashabiki na wanahabari siri ya ndoa yake na Amber Ray kuzidi kukita mizizi akisema kuwa siri ni moja tu;

“Siri ya ndoa ni moja tu, mwanamke siku zote yuko sahihi, usijaribu kumbishia,” Rapudo alisema.

Pia alimmiminia sifa Amber Ray akisema ni mwanamke anayejali. Kulingana naye, sosholaiti huyo hajawahi kumshinikiza na kwamba yuko naye kwa sababu ya mapenzi.

"Nadhani ni mwanamke anayejali. Hakuwahi kunipa shinikizo lolote. hapa nje utapata dem amekueka na pressure mingi oh nifanyie hii, but amber Ray was there for love. Kwa hivyo niligundua kuwa yeye ndiye mtu anayenifaa,” Rapudo alisema.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved