logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jackie Matubia ateta wanaume kujaza DM zake siku moja baada ya kusema yuko singo

Jackie Matubia saa anadai wanaume wengi nchini wanamtumia maombi ya kuwa na mahusiano naye.

image
na

Grafiki26 July 2023 - 09:42

Muhtasari


• Jackie alipakia video Instagram akisema wanaume walikuwa wakisubiri na kuomba mahusiano yake na Blessings kuisha ili waweza kuichua nafasi yake.

• Siku ya Jumanne, Jackie Matubia alithibitisha mahusiano yake na mpenzi wake wa zamani Lung’aho yametamatika

Jackie Matubia awasikitikia wanawake wanaowaamini wanaume.

Baada ya muigizaji wa zamani wa Zora, Jackie Matubia kuthibitisha mahusiano yake na muigizaji mwenza Blessing Lung’aho yametamatika, sasa anadai wanaume wengi nchini wanamtumia maombi ya kuwa na mahusiano naye.

Jackie alipakia video Instagram akisema wanaume walikuwa wakisubiri na kuomba mahusiano yake na Blessings kuisha ili waweza kuichua nafasi yake.

"Yooh mlikuwa mnauliza ni lini mtu akitangaza ako single, mnanijazia dm hadi email bana alaaa. Kwani ni maombi ya kazi mnatuma. Weeeuh Wanaume Wakenya mnajituma sana bana alaa. Mnanishangaza."

Matubia alisisitiza kuwa hayuko tayuri kuwa katika mahusiano ambayo yatafafanya mwanaume hyo akuwe maarufu kwa sababu ya kuwa mpenzi wake.

"Aki poleni Hio si kazi nataa tena. Aah sirudi tena, siwezi haribu muda wangu tena kujenga mtu, kumjengea jina.... Nijikute weeuh nijikutee."

Siku ya Jumanne, Jackie Matubia alithibitisha mahusiano yake na mpenzi wake wa zamani Lung’aho yametamatika baada ya muda wa zaidi ya miezi miwili ya kudokeza kuwa mambo huenda yakawa mabaya katika mahusiano yao.

Muigizaji huyo wa zamani wa kipindi cha Zora akiwaarifu wafuasi wake katika akuanti yake ya Instagram , alisema sasa anajivunia kuwa singo matha.

"Proud single mother of two," Jackie aliandika kwenye instastory yake.

Wawili hawa wamekuwa wakitoa vidokezo vya kila aina kwamba huenda mapenzi yao na baba wa mtoto wake wa pili, Blessing Lung’aho yalivunjika.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved