logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond Na Juma Jux wahesabu hasara baada ya video ya wimbo wao 'Enjoy' kufutika

Diamond Platinumuz ametangaza kwa huzuni habari za video ya wimbo wake mpya 'Enjoy' umepotea.

image
na

Grafiki27 July 2023 - 10:50

Muhtasari


• Diamond Platinumuz ametangaza kwa huzuni habari za video ya wimbo wake mpya 'Enjoy' aliyomshirikisha Juma Jux umepotea.

• Msanii huyo kupitia Instagram alipakia picha kadhaa za kuonyesha mafanikio na mapokezi ya wimbo huo na kusema kwamba katika muziki anadhani amemaliza kila kitu.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumuz ametangaza kwa huzuni habari za video ya wimbo wake mpya na Juma Jux  'Enjoy'  kutoweka.

Diamond akitangaza habari hizo za kusikitisha kupitia taarifa kwenye Instastory yake, ambapo alifichua kuwa alipokea taarifa kutoka kwa mwanamuziki mwenzake Juma jux akimfahamisha kuwa video walizokuwa tayari washarekodi,  zilikuwa tu imesalia kuzipakia Youtube zilikuwa zimefutika kwa njia ambayo haieleweki.

“Jana usiku nilipokea habari za mshtuko na masikitiko kutoka kwa Juma kuwa, Material ya video yetu ya ‘Enjoy’ yamefutika. Dah! Kuikweli nilishtuka na kuingiwa na simanzi tele.”

Hata hivyo licha ya Diamond kuvunjika moyo na habari hizo, alijipa moyo na kusema kuwa kila kitu kilikuwa mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Diamond alisema kuwa atarudia kuifanya video hizo kwa motisha zaidi hata kushinda mara ya kwanza.

“Alhamisi niko  mjini tena nakuja na nguo mpya, ijumaa tunashoot, Jumamosi inaeditiwa alfu Jumapili kabla ya kwenda kwa Zombie asubuhi chupa liko mjini.”

Msanii huyo kupitia Instagram alipakia picha kadhaa za kuonyesha mafanikio na mapokezi ya wimbo huo na kusema kwamba katika muziki anadhani amemaliza kila kitu.

Hivi majuzi Diamond alitangaza kurejea kufanya muziki kwa mpigo kama zawadi ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mama yake baada ya muda mrefu bila kutoa muziki yoyote. Baada ya tangazo hilo mmiliki huyo wa lebo ya Wasafi aliingia studioni na kuwachilia nyimbo tatu ndani ya wiki tatu.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved