Ni bayana kuwa mapenzi yanaendela kunoga baina ya mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Rayvanny na Fayvanny ama ukipenda Fahyma huku mwanamitindo huyo akijigamba kuwa sasa yeye ndiye mwanamke anayependwa zaidi duniani.
Katika ukaunti yake ya Tiktok, Fahyma huyo aliwataarifu mashabiki wake jinsi mapenzi yake na mchumba wake yanavyoendelea.
Ikumbukwe kuwa ni miezi michache tu baada ya wawili hawa kurejelea mahusiano ya kimapenzi baada ya takriban miaka mitatu kwenye kibaridi.
“Nataka kuwafahamisha kuwa mimi ndie mwanamke ninayependwa zaidi duniani kwa sasa hivi, 2023 mpaka milele. Sidhani kama kuna watu wanapendana duniani sai kama mimi na mpenzi wangu wa daima.”
Wawili hao wamekuwa wakijitokeza hadharani na kuwadhihirishia wanamitandao kuhusu mapenzi yao ya dhati. Siku chache tu baada ya kufufua mapenzi yao mwezi Aprili, Rayvanny alichorwa jina la mpenzi wake kwenye kifundo cha mkono wake.
Wawili hao walithibisha kurudi kwa mahusiano yao yaliyosambaratika takriban miaka mitatu iliyopita, siku chache zilizopita baada ya Rayvanny kumshirikisha mpenziwe huyo katika video ya wimbo wake mpya 'Forever.'
“Mtoto mbichi teketeke aki Mama umelainika. Umeumbika, acha nikumwagie sifa. Waruke sakara na mateke uzuri wako hawatofika, mama umejazisha, mikate ya kumiminisha,” Rayvanny alimsfia Fahyma kwenye wimbo huo.
Siku chache baada ya kuachia wimbo huo, bosi huyo wa Next Level Music alithibitisha wanaishi pamoja baada ya kurudiana.
Wapenzi hao walikumbwa na matatizo katika mahusiano yao mwaka wa 2020 na kutengana, baadaye Msanii huyo mahiri akaingia katika mahusiano na Paula mtoto wa Kajala kwa muda wa takirban miaka miwili.
