logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kumewakaa! Alikiba atupa makombora katika kambi la Diamond

Alikiba alimshauri Diamond kuelekeza hela zake katika masomo ya muziki.

image
na

Grafiki31 July 2023 - 06:19

Muhtasari


•Diamond alimtukana na kumdhalilisha mwenzake Alikiba hadharani katika Instastori zake akisema kuwa hakuna mwanamuziki hata mmoja aliwahi kunawiri chini ya ukufunzi wake Kiba.

• Alikiba hakuchelewa kumjibu mmiliki huyo wa lebo ya Wasafi akimlinganisha na toleo duni la mwanamuziki wa kundi la Migos, Quavo.

Alikiba amtupia bomu la moto Diamond kisa wimbo wa kura

Ugomvi baina ya wanamuziki wa Tanzania Alikiba na mwenzake Diamond Platinumz almaarufu Simba umeendela kukua huku wakirushiana vijembe mitandaoni.

Usiku wa kuamkia Jumatatu, Diamond alionekana kumtukana na kumdhalilisha mwenzake Alikiba hadharani katika Instastori zake akisema kuwa hakuna mwanamuziki hata mmoja aliwahi kunawiri chini ya ukufunzi wake Kiba.

Halafu Malkia unazungumzia roho ya kufukuta...kweli?...jamani hivi kati ya mie na wewe nani hana roho ya kusaidia watu? Wakati wewe tu mdogo wako wa damu umeshindwa kumsaidia anawiri kimuziki wakati ana uwezo mkubwa!” Aliandika Simba katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akimrejelea Alikiba.

Alikiba hakuchelewa kumjibu mmiliki huyo wa lebo ya Wasafi akimlinganisha na toleo duni la mwanamuziki wa kundi la Migos, Quavo.

Kulingana na King kiba, Diamond ni Quavo mdhaifu.

“Sema Kwevo mdhaifu sana, tu-party tuwili tutatu na marafiki, interviews kadhaa na XXL, roho inakufukuta, kutwa insta story, halafu inabidi uzoee kuhusu ngoma mfululu (Kali)🤣otherwise, Roho yako chafu itakutia stress siku uje ku-OD.” Alikiba alimjibu Diamond.

Mwanamuziki huyo aliyeachilia wimbo wake wa hivi majuzi ‘Sumu’ aliendela na kumshauri bosi huyo wa WCB kuwa hela anazotumia kupigana na wanamuziki wenzake anaweza kuzitumia vyema ikiwa angeenda katika chuo cha kufunza kuimba.

“Halafu umepata nafasi itumie vizuri mdogo wangu, hela unazowekeza kuletea figisu kwenye mitikasi ya wenzio, ungeenda hata vocal training na kuunda timu nzuri ya uzalishaji, ili uache wivu na kugandamizia.”

Alikiba alimalizia hotuba yake kwa Diamond kwa kumhimiza aisikilize wimbo wake mpya, huku akiimiminia sifa wimbo huo aliyomshirikisha Marioo.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved