Msanii Nadia Mukami amezungumzia kuhusu uwezekano wa kupata mtoto namba 2 na mpenzi wake Arrow Bwoy licha ya kudai kwamba msanii huyo bado hajafanikiwa kumtoa sokoni hata baada ya kuzaa naye mtoto mmoja.
Nadia ambaye alikuwa anazungumzua na waandishi wa habari za mitandaoni alisema kwamba amejifunza mengi kutokana na kuwa mama kwa mara ya kwanza katika maisha yake na kusema kuwa hisia ya kuwa mama inakata pande zote mbili kama msumeno- chanya na hasi.
Mukami hata hivyo alisema kuwa hatosita kufikiria kuhusu kupata mtoto wa pili pindi mtoto wa kwanza, Kai, atakapofikisha umri wa miaka 5.
“Hisia ya kuwa mama ni tamu-chungu. Lakini ni safari nzuri sana, hizo nyakati huwa nazifagilia sana. Mtoto wa pili si sasa hivi, mwenyezi Mungu akipenda nitapata wakati Kai atakuwa na umri wa miaka 5,” Nadia alisema.
Msanii huyo mama wa mtoto mmoja alisema kwamab kwa sasa anataka kujikita Zaidi katika kutafuta utajiri kupitia muziki, akisema msanii ambaye anamuiga Zaidi ni Mr Eazi.
“Sasa hivi nafuata nyayo za mtu kama Mr Eazi, kama yeye ana mradi mzima ya ujenzi wa mali isiyoweza kuhamishika Kigali nami nataka kufanya hivyo hapa Kenya, sio kitu kibaya lakini kwa sasa sitaki kuwa na fikira za mambo mengi ya kufanya,” Nadia alisema.
Mwishoni wa juma, Nadia katika kituo kimoja cha redio alidai kwamba licha ya kumzalia Arrow Bwoy mtoto mmoja, bado yeye si mke wake na kusisitiza kwamba bado yuko sokono – mguu mmoja ndani ya ndoa na mwingine nje ya ndoa – kwa kile alisema kwamba bado Arrow Bwoy hajamlipia mahari kwa hiyo yeye si mke wake rasmi.
Nadia pia katika mahojiano hayo alipata kulizungumzia hili lililozua mjadala mkali mitandaoni na kusema kuwa ulikuwa ni uvumi lakini pia akagonga pale kwenye mshono akisema kwamab utani mwingine unaweza kuwa una ukweli ndani yake.
“Arrow Bwoy anajua pia yeye, unajua mambo mengine wakati mwingine watu wanaweza fikiria kwamba unaweza sema vitu vya kumdhalilisha mpenzi wako, hapana. Unajua ni vile vitu tu mnashinda mkifanyiana mzaha kwa nyumba, pengine ndani ya nyumba anakuambia nifanyia kitu Fulani unamjibu ‘ujue hujalipa mahari’... kimzaha tu unajua. Ni mzaha tu wa mtandaoni lakini pia kila mzaha huwa na ukweli wake,” Nadia alinyoosha maelezo.