Rosa Ree awatembelea waathiriwa wa saratani Kariobangi

Haya ni kwa minajili ya kuwatia moyo waathiriwa kuendea kupambana na hali hiyo

Muhtasari

•Rapa wa Tanzania Rosary Robert Iwole, almaarufu Rosa Ree, amewatembelea watu wanaoathirika na ugonjwa wa saratani mtaa wa Karionbangi Kaskazin, eneobunge la Embakasi kaskazini, Kaunti ya Nairob.

Rosa Ree/Instagram
Rosa Ree/Instagram

Rapa wa Tanzania Rosary Robert Iwole, almaarufu Rosa Ree, amewatembelea watu wanaoguza maradhi ya saratani mtaani Karionbangi Kaskazini, eneo bunge la Embakasi kaskazini, Kaunti ya Nairobi.

Rosa Ree ambaye pia ni mwanaharakati wa afya ya kiakili, alichapisha picha zenye jumbe wa kuwaarifu mashabiki wake kuhusu ziara zake  na hafla za mwezi huu kwenye kurasa wake wa Instagram.

Hafla hiyo iliwahusisha watu wengine mashuhuri kama vile mwigizaji Eric Omondi na mchekeshaji 2mbili.

Rapa huyo alipokelewa na wenyeji ambao walimmiminia sifa. Akizungumza naye mchekeshaji 2mbili alimwambia kuwa;

"Tumekukubali huku nyumbani na tumekukaribisha."

Aliendelea kumpigia matani kutokana ka jina lake na kumwambia kuwa; "Tumeambia watu tunataka amani na  waombe rosari kwa kukukaribisha."

Hili ni jambo la kutia moyo na lennye kupigwa mfano na wasanii wengine au mtu yeyote mwenye roho ya kuwafikia wasio jiweza na wale ambao wanapitia changamoto mbalimbali kwa jamii.

Aneeleza furaha aliyonayo kwa kuwatembelea na kuungana na watu wa eneo hilo na kuwapongeza kwa juhudi walizo nazo za kupambana na changamoto za jamii.

Rosa Ree aliwaeleza kuwa si rahisi kupambana na changamoto bila imani.

"Ni vigumu sana kumwaminisha mtu, lakini pale ambapo wewe mwenyewe unaweza kusimama imara na kujiamini kiakili,kisaikolojia na kimwili inakuwa rahisi kupambana na changamoto."

Aliwashukuru washikadau wote wa kazi hiyo ya hisani na kusema kuwa , ni jambo la kupendeza kuona wakishirikiana pamoja.

"Nina furaha kuwa tumeweza kuungana na kujuana, nina furaha pia kumuona ndugu yangu Eric Omondi ambaye pia tunashirikiana pamoja na wengine hivyo kushirikiana ni jambo la muhimu katika jamii yeyote."

Eric Omondi pia alipata fursa ya kutilia uzito jambo hilo akisema kuwa yuko tayari wakati wowote kusaidia kutatua changamoto zililo kwenye jamii hasa kwa watoto na akina mama.

Hafla hiyo ilimalizika kwa kuwatunuku zawadi waathiriwa hao wa ugonjwa wa saratani kama ishara ya kuwatia moyo wa kuendelea na mapambano.