Boniface Mwangi amsherehekea bintiye aliyefikisha miaka 13 "Ni photocopy yangu!"

"Binti yangu ni 110% yangu, na tukizingatia nilivyokuwa, hatutakuwa na siku ngumu nyumbani kwetu. Yeye ni fotokopi yangu, ni kweli wanachosema, wakati mwingine mtu unajizaa mwenyewe," - Mwangi.

Muhtasari

• Mwangi alisema kuwa ujasiri wa bintiye ulimfanya kukwea mlima Kilimanjaro hadi kileleni hata kabla ya kufika umri wa mabano ya utineja.

Boniface Mwangi.
Boniface Mwangi.
Image: Facebook

Mwanaharakati Boniface Mwangi amemsherehekea binti yake ambaye amefikisha umri wa miaka 13 kama mtoto ambaye amefuata nyayo zake sit u katika sura bali pia katika ujasiri.

Mwangi alifichua kwamba binti yake amefikisha miaka 13 na kushangaa kuwa watoto kweli wanakua kwa kasi, huku akikumbuka kuwa ni juzi tu mtoto huyo alipozaliwa.

Mwangi alisema kuwa ujasiri wa bintiye ulimfanya kukwea mlima Kilimanjaro hadi kileleni hata kabla ya kufika umri wa mabano ya utineja.

“Binti yetu ana umri wa miaka 13 leo. Juzi alikuwa mtoto mdogo tu. Watoto hukua haraka sana. Yeye ni fotokopi yangu, ni kweli wanachosema, wakati mwingine unajizaa mwenyewe. A go getter, ambaye alifika Mlima Kilimanjaro kabla ya kutimiza miaka 13. Anatuletea furaha nyingi sana,” Mwangi alisema.

Kama mzazi, Mwangi alisema yuko tayari kwa vimbwanga na vitimbi vyote amabvyo huja na umri wa utineja, akisema yeye na mkewe watafurahi kupitia katika changamoto hizo kama wazazi na kuhakikisha binti yao anafika utu uzima salama.

“Kujitayarisha kwa furaha, na drama vijana matineja huwaletea wazazi wao. Tuna vijana wawili nyumbani kwetu, na wa mwisho kuzaliwa atakuwa tineja mwaka ujao. InshaAllah. Tabasamu, na machozi 🤣 yapo mbele. Binti yangu ni 110% yangu, na tukizingatia nilivyokuwa, hatutakuwa na siku ngumu nyumbani kwetu,” aliongeza.

Baba huyo wa watoto watatu miezi michache iliyopita alijisherehekea kufikisha umri wa miaka 40.

Katika ujumbe wa kuadhimisha miaka 40, Mwangi alisema kuwa ameona maana halisi ya maisha na kuahidi kuwa atazidi kujizingatia Zaidi katika afya yake ya kimwili na pia kuwa karibu na familia yake.

Hata hivyo, mwanaharakati huyo aliradidi kwamba hatolegeza Kamba katika kupigania haki za wanyonge kwani hilo ndilo jukumu kubwa ambalo alizaliwa kulitekeleza.