Mwigizaji na mwanamitindo kutoka Kenya, Brenda Wairimu amewaimiza waigizaji na wanamuziki wa Kenya na Tanzania kukumbatia ushirikiano katika tasnia ya muziki badala ya ushindani.
Amesema kwamba waigizaji na wanamuziki wa Kenya wako tayari na wamekubali kushirikiana kuliko wenzao kutoka Tanzania.
Vilevile ameongeza kuwa mashindano ni mazuri maana yanalainisha na kubaini kipi kizuri lakini ushirikiano upewe kipaumbele.
"Ushindani daima ni mzuri kwa sababu hufanya mambo kuwa bora lakini ushirikiano huja kwanza."
Akipendekeza lugha ya Kiswahili ya Watanzania alisisitiza sana ushirikiano ili kuleta matokeo mazuri katika tasnia ya uigizaji na muziki.
Siku chache tu baada ya msanii wa Kenya Nadia Mukami kupewa tuzo ya msanii bora wa kike Afrika mashariki ambayo ni tuzo ya kifahari ya AFRIMMA mwaka huu.
Mwigizaji huyo maarufu anayetambulika kwa uigizaji wake wa kupigiwa mfano,anatambulika kwa vipindi mbali mbali anavyoigiza ka vile;Monica ambapo anaigiza kama 'Monica'.
Brenda ni mtu mashuhuri na anajulikana kwa kuchukua kazi tofauti kwenye televisheni. Aliwahi kuwa mtangazaji mwenza wa kipindi cha LETS TALK katika televisheni ya Ebru.
Miongoni mwa nafasi alizochukua kwenye televisheni ni pamoja na ;Changing Times,Shareefah,Mali,Shuga,Kona, na monica.
Kutokana na ujuzi wake wa kuigiza, aliwahi shinda tuzo la Wanawake katika Filamu na kutambulika zaidi katika tamasha la Filamu la Lake International Pan African Film Festtival na kupewa tuzo za Sotigui nchini Burkina Faso,ambapo aliibuka kuwa muigizaji bora Afrika Mashariki.