Rosa Ree azungumzia uhusiano wake na Khaligraph baada ya ugomvi wao

Wakati huo huo, alikiri kwamba ugomvi wao ulikuwa kwa nia njema kwa manufaa ya aina zote mbili za usanii.

Muhtasari
  • Tukio hilo lilijiri wiki chache baada ya vita vikali kati ya wasanii wa muziki  kutoka Kenya na Watanzania.
Rosa Ree/Instagram
Rosa Ree/Instagram

Msanii na rappa kutoka Tanzania Rosa Ree amewasili nchini kwa ziara ya wanahabari pamoja na harambee ya kutoa misaada kwa waathirika wa saratani huko Kariobangi Kaskazini.

Tukio hilo lilijiri wiki chache baada ya vita vikali kati ya wasanii wa muziki  kutoka Kenya na Watanzania.

Pambano hilo lilianzishwa na Khaligraph Jones ambaye alipinga mchezo wa kufoka wa Tanzania na Rosa Ree akawaongoza Watanzania kumjibu Khaligraph Jones.

Wakati wa ziara yake nchini, rapper huyo wa Tanzania hata hivyo alizungumzia uhusiano wake na Khaligraph akisema ugomvi wa ulikuwa na maana ya burudani na kazi na haiakisi uhusiano wao katika maisha halisi.

“Nadhani tuzingatie zaidi kilichotuleta hapa. Kilichotuleta ni kitu cha amani na upendo. God is love nimekuja hapa kwa ajili ya mapenzi ya mwenyezi Mungu nimekuja hapa kufwata watu kwa ajili ya kuwatia moyo hivyo kitu ambacho kinatakiwa kituo kimoja cha kwamba kiukweli nimekuja kwa amani na upendo vitu vingine tuviache kwenye mambo ya miziki. Watu wakipigana huko mtu anatoa ngoma ngoma mwingine anatoa ngoma tunabattle kwenye kazi huku kwenye maisha tunapendana tunasambaza upendo hata ile tulikuwa tunasambaza,” alisema.

Aliongeza;

"Kuna zaidi ya maisha kuliko yale yanayokutana na macho. Kitu cha kwanza ambacho nimefanya baada ya kuja Kenya ni kitu ambacho kinatujaza sio kitu ambacho kinatujaza kwenye mitandao ya kijamii kwa hivyo kueza kuleta furaha na kutia moyo that my MO kweney mziki wangu na ndio maana ni kitu cha kwanza nilichokifanya nilipofika Kenya na mimi tutaendelea kufanya hivi ili tu kueneza upendo.”

Wakati huo huo, alikiri kwamba ugomvi wao ulikuwa kwa nia njema kwa manufaa ya aina zote mbili za usanii.

“Kile kitu kilikuja nadhani kilikuja kwa uzuri. Kwenye maisha unaeza ukawaza kitu kizuri kikaja na gear mbaya lakini at the same time pia kinakuwa kizuri,” Rosa Ree said.

 

 

 

 

Rosa Ree/Instagram
Rosa Ree/Instagram