logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akuku Danger mpya? Rapa Breeder LW afichua ndoto yake ni kuoa wanawake 200

Breeder alisema kwamba ana warembo wengi wa kimapenzi kutoka kwa angalau kila jamii nchini Kenya.

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 September 2023 - 07:07

Muhtasari


  • • "Huoni vile ninatoshana, siwezi kuwa na mke mmoja, mimi ni mtu niko na nguvu,” alisema.
  • • Breeder hata hivyo alisisitiza msimamo wake kwamba hawezi kuwapeleka wanawake katika mtoko wa kimapenzi.
Breeder LW.

Rapa mahiri wa Kenya, Breeder LW amefunguka kwamba japo yeye kwa sasa hivi hana mke, lakini ana wapenzi wa kike wengi akisema kwamba ana ndoto ya kuja kuoa wanawake wasiopungua idadi ya 200.

Akizungumza na mkuza maudhui Mungai Eve, Breeder aliakanusha kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na msanii Mandy lakini akasema kuwa mrembo huyo ni rafiki wake katika Sanaa.

Breeder alisema kwamba ana warembo wengi wa kimapenzi kutoka kwa angalau kila jamii nchini Kenya.

“Mimi unajua ni mume wa wanawake wengi, niko na mrembo katika kila eneobunge. Kila mtaa jijini nina mrembo. Kutoka kwa vijiji 12 vya Wakikuyu nina mrembo. Kusema tu ukweli nina ndoto ya kuoa wanawake 200. Huoni vile ninatoshana, siwezi kuwa na mke mmoja, mimi ni mtu niko na nguvu,” alisema.

Breeder hata hivyo alisisitiza msimamo wake kwamba hawezi kuwapeleka wanawake katika mtoko wa kimapenzi na hata hao wanawake wake 200 alisema kuwa si juu yao kukubali kuolewa naye bali yeye mwenyewe kama mwanamume ndiye ataweka sheria ya kuwajumuisha wote pamoja.

“Ili mrembo kuhitimu kupelekwa date na mimi, lazima awe chizi kama mimi. Mimi ni chizi 001 hapo Mathare. Warembo hao 200 ni rahisi kuwapata. Si Kenya pekee, niko na warembo kutoka nchi nyingi,” alisema.

Breeder alisema celebrity crush wake muda wote ni Azziad Nasenya lakini akasema kwamba atawaongeza wengine.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved