logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mohbad afukuliwa na kupatikana shingo imepinda, shuhuda asema ni pasta alipinda - video

Inaarifiwa kwamba maiti yake baada ya kufukuliwa, alipatika shingo yake imepindwa ndani ya jeneza.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri22 September 2023 - 09:45

Muhtasari


• Katika hali mpya, video sasa imeibuka mtandaoni ikimuonyesha babake nyota huyo wa muziki akiwapo huku mwanamke akieleza sababu ya shingo yake kupinda.

Moh Bad

Kifo cha mwimbaji mahiri Mohbad, kimeendelea kuibua mijadala mitandaoni ikiwa ni wiki moja baada ya kufariki na kuzikwa kwa haraka katika njia ya kutatanisha.

Baada ya maandamano kuzuka katika miji nchini Nigeria, ililazimu mamlaka kutoa notisi ya kufukuliwa kwa maiti yake na sasa hilo limeibua mjadala hata Zaidi.

Inaarifiwa kwamba maiti yake baada ya kufukuliwa, alipatika shingo yake imepindwa ndani ya jeneza.

Kumbuka kwamba picha na video zilikuwa zimemzunguka mwimbaji aliyekufa akiwa amepinda shingo yake ndani ya jeneza lake.

Katika hali mpya, video sasa imeibuka mtandaoni ikimuonyesha babake nyota huyo wa muziki akiwapo huku mwanamke akieleza sababu ya shingo yake kupinda.

Video hiyo iliyochukuliwa katika makazi ya babake Mohbad ilimuonyesha akitazama huku mwanamke huyo akifichua kwamba wachungaji ndio walioipinda shingo ya marehemu mwimbaji huyo.

Kulingana naye, wachungaji kanisani waliinua kichwa cha mwimbaji huyo ili kumwaga mafuta ya upako kama kawaida katika makanisa ya Makerubi.

Mwanamke huyo alieleza zaidi kwamba kichwa cha mwimbaji kiliinama wachungaji walipokirudisha nyuma. Mhojiwa nyuma ya kamera kisha akamwambia mwanamke huyo kwamba kila mtu anajua kwamba watu waliokufa huwa ngumu baada ya kufa. Kwa hilo, alijibu kwamba sio maiti zote ambazo huwa ngumu hivyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved