Mama yake Diamond Platnumz, anayetambulika kama Mama Dangote, amechukua hatua ambayo imeibua hisia mseto pale mitandaoni.
Mama Dangote amesitisha urafiki wake na zuchu kwenye ukurasa wake wa instagramu kwa kufuta kumfuatilia kwenye kurasa huo.
Hata hivyo Mama Dangote hajatoa sababu yeyeote iliyopelekea yeye kuchukua hatua hiyo.
Hii ni baada ya Mama Dangote kupokea zawadi kutoka kwa Tanasha Dona ambaye ni mzazi mwenza Diamond.
Ila hili linaweza kusababishwa na ujumbe ambao Zuchu alichapisha kwenye ukurasa huo baada ya kuona zawadi ambazo Tanasha alimtunuku Mama Dangote.
"Tanasha Diamond amuone tu, mzanzibar achwe tucheke." kisha akaweka emoji za mapenzi hapo.
Kwenye kurasa wake wa instagramu, Mama Dangote alichapisha video,akionyesha zawadi hiyo amabyo ilikuwa nono kweli kweli.
Alichapisha ujumbe wa kuonyesha furaha na mshangao kutokana na zawadi hiyo ya heri njema za kuzaliwa.
"Duu natoka zanhgu site, nakutana na surprise ya zawadi yangu ya siku ya kuzaliwa kutoka kwa mama Tom Kaka @tanashadonna yani sina cha klusema ila nasema Alhamdhulilahi." Alisema.
Msanii huyo Tanasha Dona alijibu jumbe huo kwa upendo akisema,
"Heri njema za kuzaliwa mama." Alisema Tanasha huku mafani wakimumiminia sifa kedekede.
Watu kwenye mtandao wametoa hisia zao kuhusiana na hili. Mtumiaji mmoja wa ukurasa wa instagramu @kizy_ala alisema kuwa;
"Ikiwa kamu unfollow basi inatokana na ujuaji wa Zuchu anajifanya kummiliki sana Diamond , wamanyema hawatakagi mke mjuaji maana wenyewe ni wajuaji."