logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aslay: kuachana na mpenzi wangu Tessy kuliniacha na machungu mno

Licha ya kutengana, Aslay amesema wanasaidiana kwa malezi ya mtoto wao

image
na

Habari29 September 2023 - 06:58

Muhtasari


•Aslay amesimulia machungu yaliyomkuta baada ya kuachana na mke wake Tessy ambaye walibarikiwa pamoja mtoto mmoja.

ASLAY/INSTAGRAM

Msanii wa nyimbo za Bongo Tanzania  Aslay jina lake kamili Aslay Isihaka Nassoro, amesimulia machungu yaliyomkuta baada ya kuachana na mke wake Tessy ambaye walibarikiwa pamoja mtoto mmoja.

Aslay alihojiwa na kituo kimoja cha runinga cha Tanzania ambapo alisimulia maisha ya mapenzi akiwa na umri mdogo wakati jina lake lilijulikana kwa nyimbo zake zilizovuma .

"Nilipokosana na mama wa mtoto wangu kwa kweli maisha yangu yalirudi nyuma kwa muda nilishikwa na msogo wa mawazo jambo ambalo lilinifanya kutotokea kwa umma kwa wakati nilikataa hata mahojiano ya moja kwa moja".Aslay alisema.

Mwimbaji huyo mashuri wa bongo alisema kilichomfanya kukumbwa na mawazo tele ni mtoto wake mdogo aliyezoea kucheza naye na wakati ndoa yake ilivunjika alizidi kukumbuka furaha na upendo wa mwanaye.

"Kwa kweli iliniuma kwa kuwa nilikuwa na malengo na mpenzi wangu ndoto yetu ilikuwa kubwa kufanikishwa maisha ya ndoa pamoja ,mke wangu alipoodoka kila siku nilidhani atarejea tena niliwatuma watu wa familia akiwemo babangu waongee naye lakini jambo ili halikufua dafu",msanii huyu aliwaambia wanahabari .

Wakati mwanahabari wa Ayo Tv alipotaka kujua mahusiano yao kwa sasa, mwimbaji huyu wa Bongo alidokeza kwamba kwa sasa mahusiano yao ni kulea mtoto tu, jambo ambalo alisema yeye pamoja na aliyekuwa mpenzi wake Tessy wanashirikiana licha ya kutengana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved