Msanii Harmonize alijawa na furaha baada ya kukutana ana kwa ana na tuktuk moja ambayo ilikuwa imechorwa picha yake kubwa kwa nyuma.
Msanii huyo alisema kwamba mpaka mtu kufikia hatua ya kuichora au kuibandika picha yake kwenye chombo chake cha usafiri maanake ni mapenzi makubwa, ya kweli na yasiyolazimishwa, akisema kwamba kitendo hicho hawezi kukilipa vya kutosha bali ni Mungu tu ndiye anaweza kulipa.
Harmonize alipakia klipu hiyo kwenye Instagram stories zake na kutoa ahadi kwamba mtu yeyote atakayechukua hatua ya kcuhora picha yake kwenye chombo chochote cha usafiri basi atakuwa katika nafasi nzuri ya kujishindia laki 5 za kitanzania sawa na elfu 30 za Kenya.
Kando na picha yake, pia alisema kwamba chombo cha usafiri kitakachokuwa na picha ya rafiki wake wa karibu Hamisa Mobetto pia mmiliki atajishindia laki 5 za ziada.
“Ikitokea tumeonana, Bajaji yako ina picha yangu basi hesabu una laki 5 [30k] taslimu. Kwa sababu siwezi kukulipa, Mungu atakulipa Zaidi. Na ndio, bajaji yenye picha ya rafiki yangu Hamisa Mobetto pia laki 5,” alitangaza.
Msanii huyo aliweka wazi kwamba wiki kesho atakuwa njiani kuzunguka ili kuona vyombo vya usafiri ambavyo vilipata uju,be huo ili kujishindia hela nyingi ambazo zinakerekete mifuko yake.
“Wiki ijayo nitakuwa ninazunguka mno kabla ya kwenda USA kwa ajili ya shoo za moja kwa moja,” alisema.
Pia Harmonize aliwashukuru mashabiki wake akisema kwamba wao ndio wamesababisha kusimama hivi tangu alipoondoka Wasafi ambapo wengi walitabiri kwamba ndio ulikuwa mwisho wake.
“Konde Gang FC Mungu awabariki nyinyi ndio mnafanya niwe hivi nilivyo,” alishukuru.
Harmonize kwa muda mrefu amekuwa akimmezea mate Hamisa Mobetto licha ya kufahamu fika kwamba mrembo huyo mama wa watoto wawili kwa sasa ni mpenzi wa mtu.
Hamisa Mobetto wiki si nyingi nyuma alimtambulisha mpenzi wake kutokea nchini Togo kwa jina Kevin ambaye ni mjasiriamali wa migahawa nchini Uchina.
Lakini licha ya hayo, Harmonize ameonekana kuwa sikio la kufa amablo katu halisikii dawa.